13/02/2024
Vijana Tumsifu Yesu Kristo!
Mama Kanisa 💒 siku ya Kesho ulimwenguni kote ataadhimisha Jumatano ya Majivu ✍️ Ambayo ndiyo mwanzo wa Kipindi Cha Kwaresma 🌝 Karibuni Sana tuone baadhi ya Mambo kuhusu Jumatano ya Majivu.
💜Jumatano ya majivu ni mwanzo wa kipindi cha kwaresima katika kanisa. Ni ishara ya kuanza kwa siku arobaini za kutafakari kwa undani fumbo kuu la upendo wa Mungu linalofunuliwa kwa kujitoa kwake na kufa msalabani, kifo cha aibu ili kuichukua aibu yetu.
💜Mama kanisa anatupatia kipindi hiki ili tuweze kutafakari njia na mienendo yetu😔
📌 *Kwanini Sasa Tunapakwa Majivu?*😊
💜Majivu ni ishara ya majuto, nayo hufanywa visakramenti kwa kubarikiwa na kanisa.
💜Tunapopakwa majivu katika paji la uso hutusaidia kutafakari na kutukumbusha kuwa wanadamu sisi tu mavumbi na mavumbini tutarudi. Hutukumbusha zaidi kuwa maisha ya hapa duniani tunapita na safari yetu itakamilika pale tutakapoungana na Bwana na mwokozi wetu katika ufalme wake😊
💜Soma; Isaya 61:3, Ester 4:1-3, Yeremia 6:26, Ezekieli 27:30, Mathayo 11:21 na Luka 10:13
📌 *KWA* *NINI* *MAJIVU* *YAPAKWE* *KATIKA* *PAJI* *LA* *USO* *NA* *SI* *PENGINEPO* ?
💜Ishara yoyote iwekwayo katika paji la uso huonesha umiliki (soma Ufunuo 7:3, Ufunuo 9:4, Ufunuo 14:1, Ezekieli 9:4-6, ).
💜Tunapochorwa ishara ya msalaba katika paji la uso ni ishara kwamba sisi tupo chini yake yeye aliyekufa msalabani kwa ajili yetu.
💜Hali kadhalika hutukumbusha ishara ya msalaba tuliyochorwa na mafuta matakatifu siku ya ubatizo wetu, hutukumbusha ahadi tuliyoiweka siku hiyo ya ubatizo na kutuita tuishi maisha ya utakatifu
📌 *MANENO* *ANAYOTAMKA* *PADRE* *YANA* *MAANA* *GANI* ?
💜Tunapopakwa majivu Padre husema; *Mwanadamu kumbuka u mavumbi na mavumbini utarudi AU Tubuni na kuiamini Injili.*
💜Maneno haya kwa upande mmoja hutukumbusha tunapoelekea, tusisikitike kwamba siku moja tutarudi mavumbini bali tuwe na furaha kwani wakati miili yetu unarudi mavumbini roho zetu zitakwenda kuungana na Mungu Baba mbinguni.
*📌MAJIVU HUTOKA WAPI?*
💜Majivu tunayopakwa hutoka katika matawi yaliyotumika katika jumapili ya matawi ya mwaka jana.
💜Majivu haya hubarikiwa na kuwa visakramenti. Hivyo majivu yanapoashiria toba