20/08/2026
Jamani amna kitu kirahisi kabisa, Kuna hii mentality watu wanayo wanahisi kuwa na biashara ndo kuwa na hela🤦🏻♀️.
Jamani kuwa na biashara ni jambo moja alafu kununua stock ni jambo la pili, Kuilipia stock ushuru ni jambo la tatu, Kuitangaza ile stock ni jambo la nne, Alafu jambo la mwisho na gumu ni kuuza ile stock.
Kuna mda mpaka unajiuliza huyu kwanini anakuja kuniomba hela wakati mm nakuwa STRONG/Najikaza haswa ili nisiseme shida zangu nijipambanie.
Kwa kifupi SINA HELA, na natamani kila mtu ajue sina hela. Hela ambazo zinazozunguka left and right ni za biashara tu. Mimi BINAFSI hata 1000 sina Bank.
alafu naumiaga sanaa mtu niliyemuweka karibu yangu akibadilika,japo nakuwaga strong mbele ya macho yao🙌🏻 ila moyoni nasali zaburi nyingi tu,Maumivu yapotee✋🏻🤚🏻