10/05/2026
THE CREATURES
(Mradi wa Siri)
Ep.... 01
Umri.... +18
Mtunzi.....GODFREY P. EMMANUELY
Tungo: Nambari 7
Maktaba: 06/05/26
mawasiliano... 0697704010
KATIKA SITU WA KOMANGAYA.
usiku wa manane mwaka 2001...
Msitu haukupumzika usiku ule.
Upepo ulipiga bila sababu. Ndege walinyamaza. Hata wadudu wale wanaolia kila usiku bila kukosa walinyamaza ghafla, kana kwamba asili yenyewe ilijua kilichokuwa kikitokea ndani ya msitu ule wa giza.
Mvua ilianza polepole. Tone moja. Mbili. Kisha kwa dakika chache ikageuka dhoruba...
mvua nzito iliyopiga majani kwa nguvu, ikafanya sauti ya vita ndogo ndogo kote msituni.
Radi ilipasua anga.
RRAAAH!
Mwanga wake mkali uliangazia kwa sekunde moja na katika mwanga huo, k**a picha ya ndoto mbaya, ilionekana banda la mbao lililosimama peke yake katikati ya msitu.
Banda zito. Banda la siri. Banda ambalo halikuwa kwenye ramani yoyote ya wilaya ile.
Ndani ya banda hilo
Kulikuwa na harufu ya damu na woga.
Wanawake saba wajawazito wamelala sakafuni juu ya magunia machafu. Mikono yao imefungwa minyororo iliyopigwa kwenye nguzo za mbao. Miguu yao vivyo hivyo. Hawakuweza kusogea. Hawakuweza kukimbia. Wangeweza tu kulala na kuomba.
Walikuwa wakilia.
Si kilio cha kelele. kilio cha kelele kilikwisha muda mrefu uliopita, usiku wa kwanza walipofika hapa, wiki tatu zilizopita.
Sasa walikuwa wakilia kwa kimya. machozi tu, bila sauti, k**a mto unaotiririka bila nguvu.
Mmoja wao mdogo kuliko wote, asiyeonekana na miaka zaidi ya ishirini alikuwa akisogeza mdomo wake bila sauti.
Alikuwa akisali. Sala yake ilikuwa rahisi. alikuwa akisali kuhusu usalama wake na mtoto aliye tumboni.
Mbele yao, alisimama mwanamume mmoja.
Alikuwa mrefu. Mwembamba kwa namna isiyo ya kawaida k**a mtu ambaye mwili wake ulifanya kazi moja tu na haukujali kitu kingine chochote. Alivaa joho jeusi lililomfikia visigino.
Usoni alikuwa na barakoa ya chuma iliyotengenezwa kwa makini. sehemu za uso zote zimefunikwa, macho tu yanayoonekana kupitia mashimo mawili meembamba.
Macho yake hayakuonyesha huruma.
Hayakuonyesha hasira pia.
Yalionyesha kitu kibaya zaidi... utulivu.
Utulivu wa mtu ambaye amefanya uamuzi wake muda mrefu uliopita na hakubali tena kuubadilisha.
Mkononi mwake alishika sindano kubwa ndefu k**a kalamu mbili zilizounganishwa.
Ndani ya sindano hiyo, kulikuwa na kioevu cheusi kilisogea polepole, kizito, k**a mafuta machafu yaliyochanganyika na kitu kingine kisichojulikana.
Akaitazama sindano kwa sekunde moja.
Kisha akawatazama wanawake.
"Usiku wa leo," alisema na sauti yake iliyofanana na chuma kinachogongana na chuma kingine.
"mtakufa nyote." alisema tena huyo mwanaume.
Mwanamke mmoja yule mzee zaidi, mwenye nywele za makaa akainua kichwa chake kwa nguvu zake zote zilizobaki.
"Tafadhali," akasema. Sauti yake ilikatika katikati.
"Daktari Kifo... muache mtoto wangu. Mimi sina hatia yoyote. Tulikuwa tu watu wa kawaida huko mtaani"
"watu wawaida?" Daktari Kifo akageuka kidogo. Kichwa chake kikainama upande mmoja k**a ndege anayesikiliza sauti ya mbali.
"Hakuna hata mmoja wenu aliyekuwa wa kawaida. Tangu mlipochaguliwa."
Akasogea mbele hatua moja ya polepole.
"Project Giza. Mnaikumbuka? Miaka mitano iliyopita sindano ile ndogo mliyopewa hospitali. Walikuambia ni chanjo. Walikuambia ni dawa ya malaria."
daktari kifo alisema mbele ya mwanamke yule mzee. Akaiinama kidogo akimwangalia kupitia mashimo ya barakoa yake.
"Ilikuwa damu. Damu ya simba. Nyoka. Popo. Na nyani. Imefichwa ndani ya mwili wenu kwa miaka mitano ikisubiri siku hii. Leo mtajifungua. Lakini hamtajifungua binadamu."
Ukimya mzito ukatua bΠ°ndani Kisha mwanamke mdogo yule aliyekuwa akisali akainua uso wake kwa mara ya kwanza. Macho yake yalikuwa mekundu ya machozi lakini ndani yake kulikuwa na kitu kingine. Moto mdogo wa hasira iliyofungwa.
"K**a utamuua mtoto wangu," akasema kwa sauti ya chini lakini thabiti, "nitakuapiza. Hata baada ya kufa β nitakufuata."
Daktari Kifo akamwangalia kwa muda.
Kisha kwa mara ya kwanza akatabasamu. Tabasamu ambalo halikuonekana chini ya barakoa yake, lakini lilionekana katika macho yake. Tabasamu baya.
"Hiyo ndiyo," akasema polepole,
"nilitarajia kusikia."
Akainua sindano.
CHWA!
Mwanamke wa kwanza alipiga yowe.
CHWA! CHWA! CHWA!
Mmoja baada ya mwingine walichomwa sindano.
Wanawake wakapiga kelele kali.
kelele zilizopanda juu ya mvua, juu ya radi, zikapotea msituni bila mtu yeyote kusikia.
Miili yao ilianza kubadilika polepole Kwa uchungu mkubwa. matumbo yakawavimba. si kwa njia ya kawaida ya kujifungua, bali kwa njia ya kitu kingine. kitu ambacho kilikuwa kikijaribu kutoka ndani kwa nguvu zake zote.
Mishipa ya shingo ikajitokeza. Macho yakabadilika rangi. ya kwanza yakawa ya njano, ya pili yakawa ya kijani, ya tatu yakawa nyekundu k**a damu.
Kucha zikaanza kukua ndefu, nyeusi, zenye makali. Meno yakatokeza k**a vile kinywa kilikuwa kidogo mno kuyashikilia.
Kisha Kimya kikatawala tena.
Kimya cha sekunde chache ambacho kilionekana k**a masaa.
WAAA! WAAA! WAAA!
Kilio cha watoto saba kikasikika kwa wakati mmoja. Lakini haikuwa kilio cha kawaida. Ilikuwa mchanganyiko. nusu kilio cha mtoto, nusu ngurumo ya kitu ambacho hakikuwa na jina.
Daktari Kifo akasimama wima.
Akatazama viumbe vipya vilivyokuwa vikilia mbele yake.
walikuwa watoto wadogo, wekundu, wenye nguvu tayari ambazo hazikuonekana kwa watoto wachanga wa kawaida.
Nyuma yao, wanawake saba walipumua mara ya mwisho. Mmoja mmoja Bila kelele K**a taa zinazozimwa na mkono usioonekana.
Daktari Kifo akapiga makofi polepole na kusema Kimya Kimya.
"Wamezaliwa, Namba moja mpaka saba. Watoto wa Giza hawa." alisema Akasimama pale kwa muda mrefu akiwatazama katika giza la banda, mvua ikiendelea kupiga nje, radi zikiangaza nyuso zao ndogo za ajabu.
Akafungua daftari lake jeusi. Akachukua kalamu.
Akaandika maneno majina saba.
Baraka. Zai. Winnie. Jini. Jocco. Sojjar. Pupwe.
Akafunga daftari..
"Miaka 25 Nitawasubiri. Na wakati utakapofika mtakuja wenyewe nyumbani." alisema daktari kifo.
ITAENDELEA