11/07/2026
Hata hii naona itakuwa ni vile vile cha msingi naona waamuzi watakao onekana wanazingua wapigwe faini na kushushwa daraja maana wanakela au mnasemaje wadau
Tanzania huenda ikaingia kwenye enzi mpya ya maamuzi ya waamuzi baada ya TFF kueleza kuwa mfumo wa Football Video Support (VS) unatarajiwa kutumika msimu ujao k**a mbadala wa VAR.
Rais wa TFF, Wallace Karia, amesema matumizi ya VAR bado ni changamoto kwa Tanzania kutokana na gharama kubwa za kuendesha mfumo huo. Kutokana na hali hiyo, TFF inaangalia uwezekano wa kutumia Football Video Support (VS), mfumo uliobuniwa na FIFA kwa mashindano yasiyoweza kumudu gharama za VAR.
Tofauti na VAR, mfumo wa VS hauna waamuzi wa video wanaofuatilia mechi muda wote. Badala yake, makocha wa timu watakuwa na nafasi nne (4) kwa kila mchezo kuomba tukio lipitiwe upya, huku mwamuzi akitazama marudio kwenye skrini na kufanya uamuzi wa mwisho.