Hajen Cosmetics

  • Home
  • Hajen Cosmetics

Hajen Cosmetics Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Hajen Cosmetics, Beauty Store, .

23/01/2026

😩 KILA UKISAFIRI NGOZI YA USO INAHARIBIKA? HII NDIO SABABU NA USHAURI! ✈️✨
Watu wengi hulalamika kuwa wakisafiri ngozi ya uso hubadilika, kuwa kavu, kupata vipele au kupoteza glow 😔
Hizi ndizo sababu kuu 👇🏽
🔹 Mabadiliko ya hali ya hewa – joto, baridi au upepo huathiri ngozi
🔹 Maji tofauti ya kuoshea uso – huleta irritation na chunusi
🔹 Kuvunja skincare routine – kuacha au kubadilisha products
🔹 Vumbi, uchafu & pollution – hufunga pores
🔹 Kunywa maji kidogo & kukosa usingizi – ngozi huonekana dull
💡 USHAURI WA SKINCARE SAFARINI:
✔️ Safiri na cleanser yako ya kawaida
✔️ Tumia moisturizer yenye unyevu wa kutosha
✔️ Sunscreen kila siku ☀️ hata ukiwa safarini
✔️ Kunywa maji mengi 💧
✔️ Epuka kujaribu bidhaa mpya safarini
✔️ Osha uso asubuhi & jioni
✨ Kumbuka: Ngozi yako inasafiri na wewe — itunze popote ulipo!
📍 Hajen Cosmetics
Tupo Tanga, Barabara ya 13 – Taifa Road
📞 0674 555 207
Karibu upate skincare bora na ushauri sahihi 💕

12/12/2025

🌸 Je unahitaji Anua toner ipi kwa ajili ya ngozi yako?
Ngozi nzuri huanza na kuchagua bidhaa sahihi. Anua wameleta toners zenye nguvu na ubora wa hali ya juu, ila kila moja ina kazi yake maalum. Hapa nimekuwekea maelezo ili ujue ipi inafaa ngozi yako zaidi ✨👇

---

1️⃣ Anua Heartleaf 77 Soothing Toner

🌿 Kwa ngozi nyeti, yenye muwasho, redness au inayowaka haraka
Toner hii ni maarufu kwa uwezo wake wa kurejesha utulivu wa ngozi. Ikiwa unaona ngozi yako inapata muwasho mara kwa mara, inakuwa red kwa urahisi au imechoka kwa kutumia bidhaa kali, basi hii ndiyo mpole sahihi kwa ajili yako. Inaondoa uvimbe mdogo mdogo na husaidia ngozi kurudi kwenye hali yake ya kawaida haraka.

---

2️⃣ Anua Rice 70+ Ceramide Glow Milk Toner

🌾 Kwa ngozi kavu, isiyo na mng’ao, au yenye ukavu wa vipindi
Hii ni k**a glasi ya maziwa kwa ngozi yako! Inajaza unyevu kwa kutumia rice extract na ceramides ambazo hujenga ukuta wa ulinzi wa ngozi. Ikiwa ngozi yako inakuwa flaky, inakosa elasticity au inaonekana kuchoka, toner hii itakurudishia ule glow wa muda mrefu.

---

3️⃣ Anua BHA 2% Gentle Exfoliating Toner

🍃 Kwa oily skin, blackheads, pimples ndogo ndogo na pores kubwa
BHA husafisha mpaka ndani ya pores. Hii toner ni mpole lakini ina nguvu ya kuondoa mafuta yaliyokithiri, kuchuja uchafu ndani ya pores na kupunguza blackheads. Ikiwa uso wako unang’aa kwa mafuta au unapata mapunye ya mara kwa mara, basi hii ndiyo choice bora kwa kudhibiti oil production.

---

4️⃣ Anua Peach 77 Niacin Essence Toner

🍑 Kwa brightening, dark spots, uneven skintone na dullness
Toner hii ni tamu k**a jina lake! Ina niacinamide na peach essence ambavyo husaidia kupunguza dark spots, kung’arisha ngozi na kuifanya iwe soft zaidi. Ikiwa unataka ile radiant peachy glow, basi hii haipaswi kukosekana kwenye routine yako.

---

✨ Kwa kifupi:
Kila toner ina kazi maalum—cha muhimu ni kuchagua ile inayolingana na mahitaji ya ngozi yako. Ukichagua sahihi, matokeo huwa haraka na ya kudumu!

---

🛍️ Products zote zinapatikana Hajen Cosmetics
📞 0674555207

07/12/2025

Je, haupati matokeo hata k**a unafanya skincare?
Usikate tamaa… mara nyingi tatizo si wewe, bali mambo madogo tu ambayo tunayasahau.
Hizi zinaweza kuwa sababu zinazokuzuia kuona mabadiliko:

✨ 1. Hutumii products sahihi kwa ngozi yako
Kila ngozi ina mahitaji yake. Ukiweka kitu kisichoendana nayo, matokeo hayatakuja.

✨ 2. Kutokuwa na uvumilivu
Skincare si uchawi wa siku moja. Matokeo mengi huanza kuonekana kuanzia wiki 4–12.

✨ 3. Kutofoata mpangilio sahihi
Cleanser → Serum → Moisturizer → Sunscreen (mchana).
Mpangilio ukibadilika, matokeo hushuka.

✨ 4. Hutumii sunscreen kila siku
Hata k**a unatumia serums nzuri, bila sunscreen matokeo hupotea.

✨ 5. Unabadilisha products mara kwa mara
Ngozi huchanganyikiwa. Ipe muda.

✨ 6. Hutumii products kwa kiasi sahihi
Kidogo sana hakifanyi kazi, kingi sana huleta madhara.

Usihofu — ukiweka misingi sawa, ngozi yako itaanza kung’aa taratibu lakini kwa uhakika ✨

Karibu tukushauri products sahihi na salama kwa ngozi yako.
📞 Mawasiliano: 0674555207

27/11/2025

Derma B Sunblock ni nzuri sana jamani!
Yaani ukitumia lazima utahadithia 🤩
Inaingia vizuri kwenye ngozi, haina mafuta, haletelezi na inalinda ngozi yako dhidi ya jua kwa muda mrefu.
K**a unataka sunscreen ambayo ni light, non-greasy na inakupa glow ya ukweli—hii hapa ndiyo mshindi! ☀️💛

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Hajen Cosmetics posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

  • Want your business to be the top-listed Shop?

Share