NLG Motivation stories

NLG  Motivation stories Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from NLG Motivation stories, Shopping & retail, Kigoma, Donetsk.

08/09/2024
Let us make it
31/05/2023

Let us make it

New Age

02/09/2022

Bahati Bukuku; ni muimbaji mkongwe wa nyimbo za Onjili nchini Tanzania ambaye amesimulia jinsi alivyolazimika kubeba maiti ya mtoto wake kwa daladala.

Bahati anasema alifiwa na mtoto wake baada ya mimba zake nyingi kuharibika, suala ambalo aliyekuwa mumewe, Daniel Basila alishindwa kulivumilia na kusababisha ndoa yake kuvunjika.

Bahati anasema; “Baada ya kujifungua mtoto wangu alifariki dunia baada ya kulazwa hospitalini kwa muda, nilijaribu kumpigia simu aliyekuwa mume wangu, lakini hakupokea simu zangu.”

Bahati anasema madaktari walikuwa wakimhimiza kulipa bili kabla ya kumruhusu kuchukua maiti ya mtoto wake ambapo bili hiyo ilikuwa ni zaidi ya shilingi milioni moja.

“Sikuwa na pesa za kulipa bili kwa hiyo nilimwambia daktari anipe maiti ya mtoto wangu au azike mwenyewe,”anasema Bahati.

Bahati anasema alipewa mwili wa mtoto wake, lakini hata hivyo alishindwa kuusafirisha kwa kukosa pesa za kukodi gari ikabidi atumie usafiri wa daladala kusafirisha maiti hiyo, tulimfunga mtoto na kushika k**a mzima, hakuna mtu ambaye angeweza kugundua kirahisi.

Bahati anasema alifanya jitihada hizo akiwa mwenyewe huku aliyekuwa mume wake akiwa bize na mambo yake.

“Tukio hilo lilinifanya nijaribu kujiua ikiwemo kunywa sumu na kusababisha kuwachukia wanaume wote kwa wakati huo, nilisimamisha hata huduma yangu ya kuimba, nilijua ndiyo mwisho wangu, lakini namshukuru dada yangu, Jenipher Mgendi alinitia nguvu na kunishika mkono nikasimama tena na kupendwa na Watanzania mpaka leo nina furaha tena,” anamalizia Bahati.

01/08/2021

HOW TO USE THE POWER OF YOUR SUBCONSCIOUS FOR WEALTH

If you are having financial difficulties, if you are trying to make ends meet,it means you have not convinced your subconscious mind that you will always have plenty and some to spare.
You know men and women who work a few hours a week and make fabulous sum of money. They do not strive or slave hard.

Do not believe the strory that the only way you can become wealthy is by sweat of your brow and hard labour

It is not so the effortless way of life is the best. Do the things you love to do ,and do it for the joy and thrill of it.

I know an executive in Los Angeles who receives a salary of $ 75,000 yearly. Last year he went on a nine month cruise seeing the beauty spots. He said to me that he had succeeded in convincing his subconscious mind that he is Worth that much money. He told me that many men in his organization getting about one hundred dollars a week ,knew more about the business than he did and could manage it better,but they have no ambition,no creative ideas and were not interested in the wonders of their Subconscious mind.

WEALTH IS OF THE MIND

Wealth is simply a subconscious convinction on the part of the individual
You will not become a millionaire by saying "I am a Millionaire,Iam millionaire

You will grow into wealth consciousness by building into your mentality the idea of wealth and abundance.

Credit: Dr. Murphy

Always do your best
15/07/2021

Always do your best

01/05/2020



AKILI NA ELIMU

Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.

Kwa mujibu wa Einstein kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Vinakuwa wazi k**a mzinga wa nyuki. Kitu pekee walichojaza kichwani ni yale waliyofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.

Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.

Manguli wa Sayansi k**a Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.

Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakakubaliana waanzishe utaratibu ambao utamuwezesha mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?

Kwahiyo mtu mwenye akili lakini akakosa elimu, ni msaada kwa jamii kuliko mtu mwenye elimu lakini akakosa akili. Mark Zukerberg hakumaliza shule lakini kwa kutumia akili amebuni mifumo rahisi ya mawasiliano kupitia mtandao.

Yeye ndiye mmiliki wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Wale maprofesa waliomuona "kilaza" darasani leo wanatumia ubunifu wake kuendesha maisha yao. K**a sio FB basi wanatumia Instagram au Whatsapp. Maprofesa wenye elimu kubwa wamezidiwa ujanja na "kilaza" mwenye Akili.

Kumbuka Einstein alisema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani. Jiulize ukiondoa yale uliyofundishwa darasani unabaki na nini? Yani ukiondoa hiyo diploma, degree, PhD au 'digrii 4' unazojivunia, kichwa chako kinabaki na nini?

K**a kuna kitu kinabakia basi hicho kinachobakia kinaitwa "AKILI". Na k**a hamna kinachobakia basi hilo bichwa halina tofauti na mtungi wa gesi.

Soma kisha SHARE na marafiki kuwafikishia ujumbe huu.

.

Dr. Anthony Campolo aliwahi kufanya stadi ya kijamii (Sociological Study) Kwa kuzungumza na watu 50 wenye umri zaidi ya ...
29/04/2020

Dr. Anthony Campolo aliwahi kufanya stadi ya kijamii (Sociological Study) Kwa kuzungumza na watu 50 wenye umri zaidi ya miaka tisini na tano.

Katika utafiti huu aliwauliza swali moja tu.
“K**a ungepewa nafasi ya kuishi tena ungefanya nini cha tofauti?”
Katika majibu waliyotoa kuna majibu MAWILI ambayo yalitawala zaidi kwa kutolewa na watu wengi.
Cha kwanza kabisa wengi walisema “ I would risk more” (Ningefanya vitu bila kuogopa changamoto ambazo zingetokea).
Wengi wao walisema pia waligundua wameshindwa kufanya mambo makubwa kwenye maisha yao kwa sababu ya uoga.
Wengi wao WALIKIRI kuwa waliwahi kuwa na mawazo mazuri ya biashara ila waliogopa kuanza kufanya.

Waliwahi kutaka kubadili taaluma zao ila walihofia kupoteza.

Waliwahi kutaka kuanza upya ila waliogopa kuchekwa.

Waliwahi kutamani kufanya kitu kitachowapa furaha ila walijawa na hofu kuwa hawataweza n.k

Walichokuja kugundua ni kuwa, maumivu waliyopata moyoni kwa KUTOKUFANYA kilichokuwa ni SAHIHI yalikuwa ni MAKUBWA kuliko HATARI walizokuwa wanaziogopa.

Na wewe unaogopa “kurisk”?
Jambo la pili ambalo wengi walilisema ni kuwa wangefanya vitu ambavyo VINGEENDELEA kuishi hata wao baada ya KUONDOKA DUNIANI.

Waligundua kuwa furaha ya kweli haiko kwenye kujipatia wanachotaka tu bali kuacha ALAMA ya kudumu duniani.

Na kuiachia dunia kitu KIZURI ambacho wataendelea KUKIFURAHIA baada ya wao kuondoka.

Waligundua kuwa sio lazima ufanye kitu kwa DUNIA NZIMA, Unaweza kuanza kwenye familia yako, kijiji chako, shule yako n.k
Amua kuwa wewe hautajutia mambo haya mawili kwa kuanza kufanya kitu leo.
See You at Top
P.S: Muda wowote ukiwa tayari kujiongezea maarifa kupitia EBooks zangu Bonyeza hapa
>>>

Linktree. Make your link do more.

13/03/2020

UHUSIANO KATI YA DAMU NA TABIA

Je unajua kuwa tabia ulizonazo ni kutokana na kundi lako la damu? Lakini pia afya yako kubwa ili uweze kuinusuru ipo.kupitia kundi lako la damu. KUJUA KUNDI LAKO LA DAMU NINJIA YA KUMALIZA MARADHI MENGI.SANA HASA YASIYOYAKUAMBUKIZA IKIWA NI POMOJA NA SUKARI,SALATANI,UZITO,.N.K

Kwa kawaida kila binadamu yuko kwenye kundi mojawapo la damu kati ya makundi manne A,B,AB na O.

Makundi haya yanaweza kutumika kufahamu tabia za binadamu na jinsi hii yaweza kuwa rahisi na ya karibu zaidi kuliko kutumia nyota “astrology” k**a ambavyo wengi wanafanya, na wataalamu wanasema tabia kwa uhusiano na kundi la damu ina uhakika zaidi kuliko wenye vyanzo vingine. Mbali na tabia, ukweli ni kwamba makundi yetu ya damu yanaweza kutuonyesha pia vile mtu anavyopendelea na asivyopendelea,

kazi anazopendelea, watu anaowapendelea na hata vyakula. Baadhi ya watafiti nchini korea wamebainisha kuwa hata namna tunavyopendelea kuketi hutegemea sana na makundi yetu ya damu, sasa tuangalie uhusiano huu

Damu kundi “A”

Hawa watu maranyingi huwa mifano ya kuigwa na wengi kwasababu ya kiu zao na upiganaji wao kwenye mafanikio, ni watu wema,wapole na wenye tabia njema. Pamoja na hayo ni rahisi sana watu hawa kupata msongo wa mawazo “stress” na kufikiria sana vitu. Wakiamua kujitoa kwa ajili ya kumsaidia mtu basi wanazama kabisa na wanaweza hata kujisahau wao.

Mazuri yao

Ni watu wanaopenda vitu vikamilike katika hali ya juu “perfectionists”, wanapenda mpangilio maalumu, wanapenda na wanaweza kuchambua mambo sawia, wanawajibika na kubeba majukumu yao,wana huruma na wako tayari kusaidia, waaminifu, ni wagunduzi, wanamaanisha, wavumilivu, na wenye tabia njema.

Mapungufu yao

Wasumbufu,wana hisia kali hata kwenye vitu vya kawaida, wakitaka kitu wametaka, wengine wana aibu,wengine wakimya zaidi na wanaopenda kujichanganya.
Kwenye maisha ya kijamii
Ni mtu ambaye unaweza kumwamini na kumtegemea
Anajali na kumaanisha
Wakati wote huepuka shari,misuguano na magomvi
Maranyingi hawapendezwi wala kufurahia sherehe zenye makelele na shangwe za ajabu ajabu,wanapendelea ukimya na utulivu.
Kazini
Unaweza kumwamini na kumtegemea katika majukumu
Wanapenda ufanisi wa kiwango cha juu kwahiyo kazi zao mara nyingi ni bora sana.
Bahati mbaya wanajali sana hata vitu vilivyo vidogo nahii huwafanya kuwa na msongo wa mawazo kirahisi.
Wasio waelewa vema watu wa kundi hili wanaweza kupata shida kufanya nao kazi
Kwenye mahusiano na mapenzi
Ni ngumu kidogo wao kufunguka na kushirikisha mambo yao.

Wanaweza kuonekana wenye aibu, au waoga.
Ukitaka kumchumbia au kuchumbiwa na mtu wa kundi ‘A’ unahitaji uvumilivu.
Wakiamua kupenda utawafahamu wakati wote na ingawa watakuruhusu ufahamu tu yale maeneoa ya maishani mwao ambayo wanajua unahusika, hawawi wazi katika kila eneo.
Ukweli mwingine kuhusu watu wa kundi ‘A’
Ni watu wabunifu na wenye ujuzi wa usanii “artists”
Wanalewa kirahisi sana, kilevi kidogo tu kitampelekesha sana
Wengi wao hupendelea kula mboga mboga “vegetarians” na ndio vyakula vinavyowafaa kwani wanatatizo la uchache wa asidi tumboni hivyo wakutumia vyakula hasa ngano vinawapa shida sana hasa katika upataji wa choo

Damu kundi “B”

Watu wa kundi hili maranyingi ni wenye tabia za kuasi na ni ngumu kuwazuia au kuwatuliza. Wanandoto na maono makubwa,wanasukumwa kwa kasi na kiu zao ingawa wanaweza kuwa wakali na wasumbufu na mara nyingine ngumu kukaa na kuzoeana nao. Wanakisimamia sana kile wanachokiamini hata k**a ulimwengu mzima usimame kinyume nao.

Mazuri yao

Wanasukumwa katika kufikia malengo yao, wako kasi kiutendaji,wanapenda raha,wana hisia nzito , wanayatazama maisha katika mtazamo chanya , wanaweza kujisimamia na kujitegemea na hawahitaji ushirika au kukubaliwa na wengine.
Mapungufu yao
Wabinafsi sana,mara nyingine wanakwepa majukumu yao,wagumu sana kusamehe,wasumbufu,wanaweza kuwa wakatitili na wenye hasira za haraka.
Maisha yao kijamii
Maranyingine ni ngumu kushirikiana nao au kuwa nao maana wanapenda kufanya mambo yao wenyewe.
Kazini
Ingawa wanaweza kuwa na malengo mengi na maono pia lakini wanaweza kuwa wasumbufu na wagumu katika kushirikiana nao kazini. Ni ngumu kufanya nao kazi maana wanataka kufanya pekeyao.
Mahusiano na mapenzi
Unaweza kufurahi nao sana kwenye mapenzi lakini uwe tayari kuvumilia hasira zao kali na za ghafla. Vumilia hali yao ya kukwepa majukumu pia,fahamu kuwa wanaweza kuwa wakali, wakatili na wasio maanisha kile wanachokisema.

Baadhi ya ukweli wa kitafiti kuhusu watu wa kundi B.

Wanatabia ya utukutu.
Pamoja na baadhi ya mazuri yao bado wanaweza wasiwe watu wazuri kwenye kuwa mume, au kuwa wapenzi wazuri kwa wasichana wao. Hii ni kutokana na urahisi wa tabia za kukosa uaminifu kimapenzi na urahisi wa kuumiza mioyo ya wengine.
Wanatabia ya kupenda wanyama “they love pets”
Wana kinga kubwa na imara ya mwili katika kujikinga na magonjwa.
Wanafurahia zaidi vyakula vitokanavyo na wanyama k**a vile maziwa “dairy products”(maziwa) n.k
Lakini hawafai kabisa kula vyakula k**a vile nyanya,kuku,karanga n.k vinawafanya wanakua na aleg mbalimbali

Pia wanawake wakitumia sana vyakula k**a ngano vinawafanya kupata hedhi mara 2 kwa mwezi

Damu kundi “AB”

Kundi hili ni watu wenye haiba mchanganyiko, hawa huwa na tabia tofauti kuanzia kuwa waoga na wenye aibu hadi wengine ni wapenda mitoko na wacheshi,wako wanafanya mambo kwa kuongozwa na mawazo na wengine hawawazi kabisa kile wanacho taka kukifanya,hii inafanya watu wa kundi hili kuwa watu wa kushangaza sana mara unapokuwa nao.

Mazuri yao

Ni rahisi sana kuwa rafiki nao.
Wanachukuliana na mazingira haraka na kwa urahisi.
Wenye kufurahisha unapokuwa nao ingawa ni watu wasiotabirika.
Wana mawazo,wana akili sana,hupenda kuweka mambo yao kwa vitendo na pia huongozwa na misimamo ya kifikra.

Mapungufu yao

Wagumu katika kufanya maamuzi.
Wanasahau sana
Ni wenye hisia za kayumba “mood swing”, mara wana furaha mara wamekasirika.
Sio waaminifu.
Ni wapinzani,wabishi na wakosaji.
Ni watu wabinafsi.

Maisha ya kijamii

Wanaweza kuwa marafiki wazuri na wenye kufurahisha.
Maongezi yao ni yenye kuhamasisha nayenye akili na kufikiria kwa hali ya juu.
Kwa kutokuwa wenye kutabirika, wengine huhofia kuumizwa kihisia au kukatishwa tamaa au kuumizwa moyo na watu hawa, hususani pale wanapokuwa sio waaminifu.
Kazini
Wanaweza kuwafurahisha na kuwapa burudani mnapofanya kazi nao lakini sio watu wa kuwategemea sana,wanaweza kukuangusha kirahisi.

Mahusiano ya mapenzi

Kuwa katika mahusiano na mtu wa kundi la damu la AB kunaweza kuwa kwenye kufurahisha,unaweza usiwena nyakati nyingi za upweke. Pamoja na haya fahamu kwamba watu hawa wanaweza kuwa wabishi na wakosoaji na maranyingine maneno yao yanaumiza. Mpenzi wa mtu au watu wa hivi lazima aelewe jinsi hisia zao zilivyo na zinavyobadilika mara kwa mara,na pale inapobidi basi uwetayari kuwapa nafasi wanayostahili ili usijiumize sana.
Baadhi ya ukweli wa kiutafiti kuhusu watu wa kundi hili.
Ni watu wazuri kwenye mambo yahusuyo fedha.
Maranyingi wanajihusisha na wanaopendendelea shuhuli za kisanaa au mambo yenye sanaa ‘arts’
Ni watu wanaoaminika kuwa wabinafsi zaidi hata katika uchangiaji wa damu,watu hawa wanaweza kupewa damu na mtu mwingine yeyote ila wao hawawezi kumpa damu yeyote isipokuwa mwenzao wa AB.
K**a walivyo watu wa kundi ‘A’ na kundi ‘B’,watu wa kundi la damu ‘AB’ hupendelea vyakula vya mboga mboga “vegetables” na pia vyakula vitokanavyo na wanyama “dairy products”

Kundi la damu aina ya O.

Hawa maranyingi wanajitahidi kuwa mahodari na mashujaa katika mambo tofauti. Mara zote kiu yao ni kuwafurahisha na kuwapendeza watu wengine ni wenye moyo wa uongozi wenye kiu ya kuwaona rafiki zao wakiwa wenye furaha wakati wote. Sio wagumu wa mabadiliko, wako tayari kubadilika, ni wenye mawazo mapana naya wazi, sio wagumu kifikra na ni marafiki wazuri.

Faida zao

Ni wenye ujasiri, wanashindana katika mambo mengi mfano mambo ya maendeleo, hufanya kazi sana na kwa bidii, ni waaminifu, wanaweza kujieleza, ni marafiki wazuri, wanasamehe, mitazamo yao ni chanya, huweza kuhisi au kuonamambo hata kabla hayajatokea,wanakiu ya kufahamu na kudadisi na pia niwatu wema na watoaji.

Mapungufu yao

Maranyingine wanaweza kuwa wenye fujo, wanaopenda sifa, wanavutia vitu upande wao, wanaepuka au kukwepa majukumu,unaweza kuona hawa wanaigiza mambo, wakitaka wametaka hadi wapate na nirahisi kuwaondoa kwenye kile wanachokifanya “easy to be distracted”.

Maisha ya kijamii

Ni marafiki wazuri na unaoweza kuwategemea, ni waaminifu, ni wawazi,ingawa mara nyingine wanaweza kukuudhi, pia wakati mwingine wanatamani kusikilizwa wao tu.
Kazini
Wana kiu ya mafanikio, hufanya kazi kwa bidii ingawa kukatishwa tamaa na kupoteza hamasa ya kazi kirahisi sana. Mara nyingine ili wafikie malengo ni vema wakisimamiwa kwenye kazi wanayo fanya badala ya kuachwa wafanye wenyewe..

Mahusiano ya mapenzi

Ni watu wenye mvuto wa kimahaba pia watu hawa wana hisia Kali za kimapenzi wanaweza kuonyesha mapenzi kwa wale wanaowapenda ila ni vema ukafahamu kuwa watu hawa hutarajia upendo wa jinsi ile ile wao wanavyoonyesha upendo kwako bila hivyo utakosana nao.

Ukweli wa kitafiti kuhusu watu hawa

HAWAPATI MARADHI KIRAHISI
Kwanza ifahamike kuwa watu wenye damu kundi hili wamegawanyika mara mbili ambazo ni damu kundi “O” chanya (O positive) na kundi “O” hasi (“O” negative) mgawanyo huu umetokana na mgawanyo wa kitaalamu ambao huitwa “rhesus factors” ambao ndio unaotumika kugawanya makundi ya damu.
Kwa ujumla kundi hili la damu liwe hasi au chanya halina proteins maalumu zilizomo ndani ya damu ambazo huitwa “antigens”(ndio maana wanashauri vyakula vya protean kwani hata katika kuondosha uzito wao vyakula vya protin vinafanya vema zaidi) ambazo ndizo mara nyingi ni rahisi kushika magonjwa isipokuwa lina “antibody” ambazo ndizo kinga mwili zinazopambana na maradhi ndiyo maana damu kundi “O” linaitwa “Universal Donor” damu kundi lolote linapokea.
Na kwa wakati fulani maradhi yanayowasumbua watu wenye damu kundi hili ni malaria, kichwa na mafua na wengine husumbuliwa sana na ugonjwa wa kutoka damu za pua (Rhinits) au wengine huita kambaku ambao husababishwa na kula nyama yenye lehemu nyingi (cholestrolel) ambazo ni nyama ya ng’ombe, kondoo, samaki aina ya dagaa, uwono na mboga ya majani inayoitwa kisamvu na wakati mwingine maziwa ya ng’ombe au kutembea kwenye jua kali sana au kutumia manukato yenye harufu kali.

NI WAPENDA NGONO

Watu wenye damu kundi hili wana hisia kali sana za mapenzi hii ni kutokana wana homoni nyingi, hali hii inawapelekea kupenda sana ngono na vile vile huwa wakizaa wanafanana sana na watoto wao iwe sura, tabia au mwendo iwe mwanamke au mwanaume
Watu hawa Mara nyingi huwashwa masikio yao kwa ndani hivyo Mara nyingi wanajikuna masikio
Wanaaminika huwa na tabia za kijeshi.
Wengi wao kwa asili ni watu wa kupenda michezo.
Wanaaminika kuwa watu wema na waliotayari kusaidia mtu yeyote, hata katika uchangiaji wa damu ‘watu wa kundi ‘O’, wanaweza kumpa damu mtu mwingine yeyote.
Wanapendelea na kujisikia raha wanapokula nyama “meet lovers”.

To a maoni yako

Maada hii ndefu sana kwani inaweza kukufanya ukapungua UZITO WAKO ,UKATATUA CHANGAMOTO ZA SUKARI,PRESSURE,SARATANI maadamu ujue mpango wa chakula cha kundi la damu

Kwa ushauri na maoni wasiliana nami kwa whatsapp no +255743358024

Michael Jackson alikuwa ni binadamu mwenye ndoto nyingi lakini Ndoto zake 2 kuu maishani zilikuwa ni:1. Kwanza ni kuwa m...
18/08/2019

Michael Jackson alikuwa ni binadamu mwenye ndoto nyingi lakini Ndoto zake 2 kuu maishani zilikuwa ni:

1. Kwanza ni kuwa mwanamziki mkubwa zaidi duniani wa Pop.

2. Kuishi miaka 150.

Baada ya kuifanikisha ndoto yake ya kwanza kwa ufanisi mkubwa akiwa na miaka 25 tu aliamua kuanza kuwekeza kwenye ndoto yake ya pili ambayo kwa wakati huo ilikuwa ndiyo takwa lake kubwa.

Ili aweze kuishi miaka 150 (Karne moja na nusu) aliamua kufanya mambo yafuatayo:

1. Aliajiri madaktari binafsi 12 wa kumchunguza mwili wake wote hadi nywele na kucha kila siku.

2. Ilikuwa ni lazima chakula chake kipitie maabara kupimwa kabla hajala.

3. Aliwaajiri wataalamu 15 kufuatilia mazoezi, kazi na kila jambo alilofanya kila siku.

4. Alitengeneza kitanda maalumu kilichokuwa na uwezo wa kufanya 'regulation' ya hewa.

5. Watu 50 waliwekwa tayari kujitolea viungo vyao k**a angepata dharura yoyote. Aliwalisha watu hao, aliwatunza na kuwalipa mshahara kila mwezi kwa kazi hiyo.

Baada ya kufanya hayo alikuwa na uhakika wa kuishi karne moja na nusu bila mashaka yoyote. Lakini June 25, mwaka 2009 akiwa na miaka 50 tu moyo wake ulizima ghafla na ndoto yake ikawa imefika mwisho.

Timu ya madaktari wake bingwa 12 haikuweza kuzuia pumzi yake isiondoke. Wale watu 50 waliowekwa 'standby' kumpa viungo hawakuweza kumsaidia. Akazima ghafla k**a taa ya umeme iliyoishiwa luku.

Pamoja na juhudi za madaktari wengine kutoka Calfornia na Los Angeles hawakuweza pia kuokoa maisha yake. Mtu ambaye kwa miaka 25 alikuwa hawezi kunyanyua unyayo wake bila ushauri na ruhusa ya madaktari akawa kafika mwisho bila kutimiza ndoto yake ya kuishi miaka 150.

Safari ya mwisho ya Michael Jackson ilishuhudiwa moja kwa moja na zaidi ya watu milioni 3, rekodi ambayo haijavunjwa hadi sasa. Ndiye mtu aliyepata kuagwa na watu wengi zaidi katika historia ya dunia tangu enzi za Pontio Pilato.

Siku aliyofariki mitandao mikubwa ya Wikipedia, Twitter, Yahoo, AOL's instant messenger ilielemewa na mzigo wa watumiaji waliokuwa wakisaka taarifa za kifo hiki hadi ikaacha kufanya kazi. Google pia ilivunja historia ya matumizi yake kwa siku ile.

Michael Jackson alitaka kupambana na kifo lakini hakuweza hata kufikia nusu ya umri aliopenda kuuishi. Mtu aliyekua na uwezo wa kufanya lolote ili aweze kuishi umri autakao lakini alizima k**a mshumaa. Biblia inasema ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? Hakuna. (Mathayo 6:27).

Ikiwa hatuwezi kuongeza hata kimo chetu basi hatuwezi kufanya lolote kuhusu hatma ya maisha yetu. Michael Jackson alifanya yote yaliyowezekana ili aishi miaka 150 lakini hakufika hata nusu ya umri huo. Lakini kuna mzee asiye na uhakika wa milo mitatu kule Tandahimba, Rombo, Ngara au Tukuyu ameishi umri mkubwa hata mara mbili ya Michael Jackson. Ni kwa neema tu.

Uhai na uzima tulionao ni zawadi kutoka kwa Mungu. Sio kwamba tunastahili kuliko wengine, hapana. Sio kwamba tumejitunza kuliko wengine. Hapana. Ni kwa neema tu. Hata hatma ya maisha yetu vipo mikononi mwa MUNGU mwenyewe.

Ishi kwa upendo na kila mtu. Ukipata madaraka usiyatumie kunyanyasa wengine. Usifunge watu bila hatia, usiue wapinzani wako, usipoteze wanaokukosoa. Damu zao zitakulilia daima na siku ya mwisho utaulizwa.

Hapa duniani hatuna mji udumuo bali sote twautafuta ule ujao. Ishi kwa amani na watu wote. Maandiko yanasema mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi (Ayubu 14:1). Tumuombe Mungu atuepushe na kiburi, atufundishe kuzihesabu siku zetu na kutujalia mwisho mwema.!.....

23/06/2019

IJUWE HISTORIA YA KABILA LA WAHA NA UHUSIANO WAO NA WATUTSI:

MKOA WA KIGOMA
Takwimu ya wakazi mwaka 2014 jumla ya wakazi wa mkoa huu walikuwa zaidi ya milioni 2.1 Mkoa wa Kigoma umepakana na nchi ya Burundi , mkoa wa Kagera na Geita upande wa Kaskazini, Mashariki umepakana na mikoa ya Shinyanga na Tabora, Kusini umepakana na mkoa wa Rukwa na kwa upande wa Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo.

Wakazi wa asili wa mkoa huu ni wa Kabila la WAHA. Inazo wilaya 6, Tarafa 21, Kata 136, mitaa 176 na vitongoji 1,856 na kufanya jumla ya halmashauri za Wilaya kuwa 8; Kakonko, Kibondo, Kasulu mjini, Kasulu vijijini, Buhigwe , Uvinza, Kigoma vijijini na Manispaa ya Kigoma /Ujiji.

UKUBWA WA ENEO;
Ni KM2 45.066(sawa na 4.8) ya eneo lote la Tanzani ambapo KM2 8.029 ni maji na KM2 37.037 ni Nchi kavu. Kwa ujumla eneo la mkoa wa kigoma ni Tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB Kribu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750.

MAKABILA;
Mkoa huu unayo pia makabila mengine k**a, Wabembe, Wahutu, Watongwe,Wagoma , Wabwali , Wamanyema, Waholoholo na Watutsi.

Wapo pia makabila mengine kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wanaoishi k**a nyumbani kwa kuhamia ama kwa kufanyakazi tu kisha wakiwa na mipango ya kurudi katika mikoa yao.

KABILA LA WAHA;
KABILA LA Waha; Jina la Kabila ni WAHA. Watu wa kabila hili huitwa Waha au Abhaha katka wingi na katika umoja Umuha. Lugha yao ni miongoni mwa familia ya lugha za Kibantu iitwayo Kiha. Hapo zamani himaya yao kiutawala iliitwa Buha ambayo ilijumuisha mipaka yote ya eneo la mkoa wa Kigoma uliopo Kaskazini –Magharibi mwa Tanzania kwa jina maarufu Buha (Kigoma Mwisho wa reli).

Kwa mujibu wa Mchambuzi na Mwandishi wa masuala ya Kihistoria Bwana B.A Ogot, katika kitabu chake kiitwacho “A Survey of Two Thousand years of East Afrikan History “ katika ukurasa wa 76 -85 amejaribu kuorodhesha jumla ya makabila yaliyoishi katika eneo la Afrika Mashariki kwa kuzingatia lugha na maeneo yao. Hapa ni wazi kwamba jamii za watu wa zamani ziliishi kwa kuhamahama katika nyakati tofauti tofauti zikitokea sehemu za Afrika Magharibi kandokando mwa mto Niger na Kongo, na jamii nyinginezikitokea maeneo ya Afrika Kaskazini hivyo hadi kufikia miaka 1300 KK tayari jamii za Wabantu zilikuwa zimeshafika katika eneo hili la Afrika Mashariki. Nitaje tu baadhi ya makundi ya wabantu yaliyoishi pamoja katika koo zao na koo za Waha katika eneo waliloishi linalozunguka Ziwa Viktoria walikuwa ni; Wajita, Wakerewe, Wakara, Wazinza, Wahaya, Wahutu na Watwa, Wakiga, Watoro, Wanyoro, Wanyankole, Waganda, Wasoga, Wasese, Wakwere, Wakenyi, Wagisu, Wasiriani, Waluya, Wasubi, Waha, Wahangaza, Washubi na Wavinza.

Katika eneo hili ndipo walipofikia Wabantu hawa wa mwanzo na kuweka makao yao na hivyo hawakuwa katika makabila haya tuyaonayo sasa, bali ilikuwa katika makundi madogo madogo tunayoweza kuyaita koo.

Kadri walivyoendelea kuishi kwa muda mrefu waliongezeka kisha waliendelea kujigawa kwa kuhama na kwenda kuishi katika maeneo mbalimbali ya Afrika Mashariki hadi katika maeneo wanayoishi hadi hivi sasa.

Hadi kufikia karne ya 16 tayari koo za Waha zimeshafika katika eneo la Buha na kuishi pamoja katika maeneo tofauti toufauti. Waha hutambuliwa kwa koo zao ambazo zimesheheni utamaduni wao katika mila na desturi zao, misemo, hadithi, ngoma, mtindo wa mavazi, nyumba zao, vyakula vyao na mtindo wa kuabudu.

Aidha pia koo hizi katika kujitofautisha na koo zingine ziliweza kujiita majina tofauti tofauti na kutumia majina ya wanyama na ndege mbali mbali k**a; Tumbili, Nguruwe, Nyati, Hondohondo, nk. Pia ilikuwa sio jambo geni kwa ukoo mmoja kujitenga na ukoo wake na kujiita aina nyingine ya mnyama tofauti na Yule wa awali kwenye ukoo huo ingawa ukoo uliweza kubakia uleule wa mwanzo na sababu ziliweza kubainishwa. Kwa mfano, Wakimbili Hondohondo na Wakimbili Mpongo na wakimbili Vinza .

Shabaha kuu ya kufanya hivyo ilikuwa ni kujitofautisha baina yao na koo zingine. Baadhi ya koo za kabila la Waha ni k**a; Wajiji, Wakimbili, Watela, Walagane, wanyongozi, Watambo, Wasindi, Walima, Wasase, Waheza nk. Moja ya sifa maarufu ya kabila hili ni ile ya kuhama na nyumba na methali yao isemayo ” Ibhiharagi bhisumbinyama” yaani Mboga ya maharage ni bora kuliko nyama. Ikiwa na maana kwamba “Bora kutumia mboga ya maharage inayopatikana kwa urahisi kuliko kupenda nyama iliyo ya ghali na isiyopatikana kwa urahisi”

WAHA NA MFUMO WAO WA UTAWALA; Kuna usemi wa Wazungu usemao kwamba “Mwafrika hakuwa na maendeleo yoyote kabla ya ujio wa Wazungu” na Kuna pia msemo wa watu kwamba ” Waha hawakuwa na tawala zao kabla ya ujio wa Watutsi”.

Kauli hizi si za kweli, kwani binadamu amekuwa akipambana na mazingira yake kwa miaka milioni 30 iliyopita. Kwanza tuone dhana ya ” uongozi” ni mamlaka au karama ya kuonyesha njia kwa vitendo. Dhana ya “UTAWALA” Neno hili lina maana pana kulingana na aina zake, kwa kifupi Utawala ni “Mfumo unaotoa Mamlaka ya dola au serikali kwa kiongozi.”

Hivyo kutokana na dhana ya Uongozi na Utawala hapo juu, ni wazi kwamba kila palipo na watu kuanzia wawili na kuendelea kuna utawala au Uongozi. Kwa hali hii Waha waliishi mwanzoni katika koo mbalimbali zilizokuwa na mfumo wake wa uongozi. Mfumo maarufu uliotumika kutawala katika jamii ya Waha ilikuwa wa UKOO. Koo zilizoishi katika eneo moja ziliwpaswa kuchagua ukoo mmoja na kuusimika kuwa ukoo wa utawala wao , hivyo mtawala alitokea katika ukoo huo. Koo tawala ziliitwa kwa jina moja la WATEKO katika wingi na katika umoja UMTEKO. Mfano mmojawapo wa koo hizi za utawala ulikuwa ukoo wa Wajiji uliotawala katika eneo la NKalinzi au Kalinzi ya leo ikianzia sehemu za Mukigo.

Ili Mteko/Wateko aweze kutawala alipaswa kuwa na sifa mbalimbali k**a; uwezo wa kutoa tiba, kuleta mvua, uwezo wa kuongoza watu kwa hekima , uwezo katika shughuli za ulinzi na usalama, uwezo wa kuleta neema miongoni mwa jamii yao na kulinda ardhi nk.

Mfano wa pili wa ukoo wa wateko ulikuwa ukoo wa Wakimbil wa Manyovu-Ibhugalama (Kibila) ukoo huu ndio ulikuwa ukiongoza katika sehemu hizo kwani tunaona kwamba hata wakati mfumo wa utawala wa Wami ukoo huu na maeneo yake ndiyo yaliyochukuliwa kuwa makao makuu ya viongozi (umtwale Munini/ watwale) na katika kipindi cha matambiko inasemekana shughuli zlikuwa hazifanyiki hadi ukoo wao umehudhuria .

Hivyo koo za Waha zimedumu na kuishi kwa zaidi ya miaka 1600 katika koo zao huku baadhi ya koo zikiwa ndio watawala( Wateko) wa koo zingine hadi mfumo wao ulipobadilika kutokana na ujio wa jamii ya Wahima/Watutsi ambao walifika na kuanzisha mfumo mwngine wa utawala katika karne 17 miaka 1700 BK iliyopita. Katika miaka hiyo eneo lote la Buha lilikuwa na kabila moja tu la Waha lililoishi hapa. Hivyo ujio wa Watutsi ndio uliopelekea mwingiliano wa kwanza wa jamii ya watu wasio Wabantu katka ukanda huu wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Kadhalika na katika sehemu zingine ambako Wabantu walihamia k**a; Urundi, Rwanda, Karagwe, Bukoba na Ngara, Ukerewe, Wazinza nk. Waliendelea kuishi katika mifumo ya Tawala zao hadi pale walipoingia katika mabadiliko kadri ya historia yao. Kwa makabila niliyoyataja nitajaribu kuelezea jinsi walivyoathiriwa na ujio wa jamii nyingine katika maeneo yao.

MUUNDO WA UTAWALA;

Katika tawala za Wateko sikuweza kupata muundo wa uongozi ulliotumika katika kutawala. Sababu ni kwamba, mfumo wao ulitumika kwa muda mrefu na hakukuwa na Masimulizi au maandishi yaliyoweza kuandikwa kwa ajili ya kuweka kumbukumbu. Hata hivyo Historia ni somo linalokubali mabadiliko hivyo ni fursa kwa wasomaji na wachambuzi wengine wa mambo ya kihistoria kuichukulia k**a mahali pengine pa kufanyia utafiti ilikuja na majibu ya uhakika kwa ajili ya kutoka elimu kwa kizazi kilichopo na kijacho.

8.KABILA LA WATUTSI.

Watutsi au Wahuma au Wahima au Wahinda au Imfure, Banyaruguru =Rwanda watu wa kaskazini), Wahima=Burundi, Banyamlenge=sehemu za Kivu kongo, Watutsi= Buha, Bahinda=Karagwe yote haya ni majina yao. Majina haya yametokana na mtindo wa jamii ya Wabantu kushindwa kuwaita kwa maneno yao mfn. “Wa’o’oruma’ kwa kibantu WAHIMA /WAHUMA, kutokana na kushindwa kutamka majina yao yanayotamkwa kutokea Puaani na kooni. Hili Ni kundi la jamii nyingine ya watu wa Afrika Mashariki lililotokea katika eneo la Afrika Kaskazini sehemu za Chari-Naili kandokando mwa mto Naili katika karne ya 17 au miaka 1700BK.

Tofauti na kundi lile lilotoka katika eneo la Afrika Magharibi la Wabantu. Kundi hili lipo katika jamii ya kundi linalozungumza lugha za Wamoru Madi, Waniloti au Waafroasia. Kundi hili k**a yalivyo katika makundi ya kibantu yalijimega na kuhamahama. Kwa kuwa yalikuwa makundi ya wafugaji walisafiri katika makundi madogo madogo mno hasa ya mtu mmoja mmoja au familia.

Hii iliwezekana kutokana na mtindo wao wa ufugaji ambao uliwawezesha kufika mahali na kukaa kipindi kirefu wakichunga ng’ombe zao, tofauti na Wabantu ambao wengi wao walikuwa wakulima hivyo pindi walipoamua kuhama walihama na kuishi katika makundi makubwa ya ukoo na kuendeleza shughuli zao za kilimo.

Jamii hii ya watu ilifika katika makundi madogomagogo katika vipindi tofauti tofauti hadi maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania katika Bukoba,Ngara, Unyamwezi na Buha na katika tawala za Urundi na Rwanda kwenye nchi za Burundi na Rwanda wakitokea sehemu za Uganda.

Ushahidi unaonesha hivyo kutokana na baadhi ya jamii hizo kuonekana zaidi ukanda huu tofauti na ilivyo katika mikoa ya Mara, Shinyanga Mashariki na Kaskazini, Dodoma na ama katika mikoa ya kusini na pwani ya Tanzania. Pia jamii hii haina lugha yao maalumu wanayozungumza.

Kwa kuwa hawa sio jamii ya wabantu tungetarajia waongea Lugha k**a za Kimasai ama Kijaruo na zinginezo zinazozungumzwa na jamii ya watu waliotokea Kaskazini. Badala yake huongea lugha za Kibantu.

Kabla ya kutazama utawala wao hebu kwanza tuone namna walivyoanza kuishi na jamii za Wabantu walizozikuta. K**a nilivyotambulisha hapo awali kwamba, wabantu waliendelea kuishi katika tawala zao za kiukoo, zikifanya shughuli zao. Walipofika hawa Watutsi kwanza walijitambulisha kwa Mteko aliyekuwa mtawala. Kisha walitambulishwa kwa ukoo wa Wateko na kwa baadaye kwa koo zote ziLIzoongowa na Mteko. Baada ya wenyeji kuridhika na kuwapokea katika himaya yao, Watutsi kwanza waliomba kuingia katika koo za Wateko k**a watoto na ndugu wa Ukoo.

Ndio maana hadi leo huwezi kukuta ukoo ama kabila la Watutsi , bali wameendeleza koo za wateko pale wanapojitambulisha kwa koo za wenyeji kwa kuzingatia mahali walipo. Kisha sehemu ya mali zao (ng’ombe) zilitolewa kwa mtawala wakimaanisha kushukuru kukubaliwa kwao ndani ya ukoo husika. Katika kuishi kwa muda mrefu jamii hii iliendelea kuaminiwa na kukubalika katika koo, hivyo shughuli na michakato yote ya Kifamilia na kiukoo zilihusisha pia watutsi wakiwa sehemu ya ukoo .

lli kuhakikisha kwamba wanawateka wenyeji na kutwaa Utawala mbinu kadhaa zilitumika;mfn, Kuozesha watawala binti zao, Mvuto kutokana na maumbile yao (uzuri wa umbo), mfumo wa Ubugabile, Wanawake kuua waume zao hasa wale waliokuwa watawala ili watoto wa Kitutsi walithi utawala, tabia za kujifanya wanyenyekevu, heba za kuwa na malingo Fulani ambazo zote hizo ziliwavutia jamii za Watawala na wanaukoo kwa ujumla wao.

Katika masimulizi nimewahi kusikia kwamba ilifika mahali baada ya Watutsi kukaa na Jamii ya Wabantu Wanyamezi hadi leo wameweza kuziishi baadhi ya Tabia zao. Hasa za majivuno na malingo. Baada ya kuhakikisha kuwa wameweza kuaminiwa na jamii yote kwa wema waliokuwa wakiufanya na kwa sababu hizo ndipo jina la Mtutsi liliipata sifa likimanisha MTU MWEMA . Kumbuka maneno k**a” Mtutsi wanje” Likimaanisha ; Mtu mwema kwangu. Ni msemo ambao hadi leo kwa baadhi ya maeneo ya Buha umekuwa ukitumika . Zoezi hili lilifanyika kimkakati, kwa makini na kwa kipindi kirefu .

K**a tunavyofahamu kwamba mtu wa hila huwa hakurupuki katika kutekeleza mipango yake.

MFUMO WA UTAWALA WA WAMI;

Utawala wa Watutsi ndipo ulipoanza Baada ya kufanikiwa kuuangusha utawala wa Wateko/ Umteko katika karne hiyo ya 17BK. yaani miaka 1750BK katika sehemu za Urundi na Rwanda na katika miaka ya 1700BK. katika eneo la Buha, kwa kumpa jina mtawala wao kuwa ni MWAMI. Mwami katika tofasili isiyo rasmi ya Kibantu ni mtawala /Kiongozi/ Mfalme mwenye hadhi ya juu kabisa.

Mfano wake ni Mungu “Umwami wachu wo Mwijuru” Hii ni nukuu ya baadhi ya maneno ya sara za Kanisa Katoliki katika lugha ya KIHA, ikimanisha “Mungu wetu uliye mbinguni”.

WAMI; Baada ya kuanguka kwa utawala wa WATEKO ndipo Wami waliposhika madaraka ya utawala . Shughuli kuu tatu na muhimu ndizo zlizobakia kwa Wateko. Shughuli hizo zilikuwa ni kumiliki na kugawa ARDHI, MATAMBIKO NA DINI.

Mambo ya ulinzi na usalama, utawala, mahusiano na nchi za nje na mambo ya ndani nk. yalikuwa chini ya utawala wa Watutsi. Hapa sababu zilizopelekea kuchukua utawala kwenye maeneo hayo, ilikuwa ni kwamba, wafugaji walizoea kuwa na jeshi linalolinda mifugo yao hivyo waliona ni muhimu wadhibiti masuala ya ulinzi na usalama wa mipaka yao.

Aidha pia kwa kuwa jamii zao ndiyo waliotawala karibu maeneo mengi baada ya mfumo wa utawala wa Wateko kuanguka wangependa kushirikishana masuala yanayohusu habari za nchi zao ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wan chi zao hizo. Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki
Waha walianza kupoteza umaarufu wao wa Mfumo wa Utawala wa UKOO/ WATEKO.

Mfumo wa Watutsi ulichukua nafasi na Buha ikaangukia katika mikono ya watawala wa Mwami. Katika nyakati tofauti tofauti Tawala ziliundwa katika eneo lote la Buha. Tawala zilizoanzishwa katika eneneo lote la Buha zilikuwa 6 kwa majina yao ni;i;UTAWALA WA HERU=Ikulu yake HERU JUU pamoja na sehemu ya mipaka yote ya Manyovu, Kasulu vijijini na Kasulu Mjini,ii; MUHAMBWE=Ikulu yake KIBONDO na sehemu za Wilaya ya Kibondo,iii; BUYUNGU= Ikulu yake KAKONKO na sehemu za mipaka yote ya wilaya ya Kakonko na iv;UJIJI=Ikuu yake Nkalinzi na sehemu zote za mipaka ya wilaya za Kigoma vijijini, Manispaa ya Kigoma/ Ujiji na wilaya ya Uvinza .

Nyingine zilizomeguka kutoka kwenye utawala wa Heru ni; v;NKANDA-LUGURU=Ikulu yake NKANDA na maeneo yote ya mipaka yake na vi;HERU-USHINGO=Ikulu yake Heru Ushingo.
MUUNDO WA UTAWALA WA MWAMI;
1.Mwami-Mteko
2.Umtware Munini
3.Umtware Mtoyi
4. UMhamagazi
5.Katikiro
6.Abhintala

MUUNDO WA UTAWALA WA MTWALE MUNINI
1. Umutware Munini.
2. Umutware Mtoyi.
3.Umhamagazi(mtoa Taarifa).
4.Katikiro(askari).
5.Abhintala(wananchi).



UTAWALA WA HERU; mwaka 1750 – 1963;

1. MWAMI RUHINDA; Mtawala wa kufikilika anayedhaniwa kuwa ndiye mwanzilishi wa Himaya zote za Wahinda.
2. MWAMI KANYONI.
3. MWAMI NTARE I.
4. MWAMI BIGONDA.
A. MWAMI GWASA I === wa Nkanda-Luguru na Heru- Ushingo zilizojitenga kutoka Utawala wa HERU.
5. MWAMI NYAMIHONDO====GWASA I, aliyetawala HERU katika karne ya 18.
6. MWAMI KANYONI II.
7. MWAMI NTARE II ===Aliongoza vita dhidi ya Wangoni na Watemi wa Wavinza katika miaka 1850.
8. MWAMI GWASA II ===Aliongoza vita dhidi ya Wajerumani katika mwaka 1897.
9. MWAMI NTARE III ===Alifariki wakati wa mapigano baina ya Wami wa Buha 1918.
10. MWAMI KATONDWA ===alijisimika kuwa Mwami lakini aliondolewa na WATWALE na kumsimika MWAMI TUNDA.
11. MWAMI LUYAGWA ===Alitumia majina ya Gwasa, Ntale na Ruhinda.
12. MWAMI KANYONI III ===Alisimikwa na wakoloni wa Kiingereza k**a kibaraka wao
13. MWAMI NTARE IV ( TERESIA JOSEPH NDALICHAKO)=== Ni Mwani mwanamke wa kwanza na wa mwisho kutawala HERU mwaka 1949 -1963. Ana sifa ya kuoa na kumtolea Mahali mume wake kutokana na MWAMI haolewi na kucha nchi yake.

Utawala huu ulichukua eneo lote linalopakana na Mto Malagarasi kuanzia mipaka yake ya Magharibi na Kaskazini na mipaka yake ukivuka Mto Maragalasi katika maeneo yanayopakana na wilaya za Kibondo, Kasulu na Uvinza. Aidha pia mipaka yake ya Kusini kwenye mipaka ya wilaya za Uvinza na Kigoma Vijijini.

Katika kipindi hicho idadi ya watu ilikuwa ndogo hivyo sehemu kubwa ya eneo lake ilikuwa pori. Mtawanyiko wa watu ulikuwa k**a ifuatavyo; Heru, Manyovu, Ushingo na Nkanda. Pia tunapotaja sehemu ya utawala tusidhani kwamba sehemu yote ya eneo tulionalo hivi leo, au tunalosikia kwamba ilikuwa himaya ya utawala Fulani kwamba ilikuwa imeenea watu la hasha, kilichokuwa kinafahamika ni mipaka yake tu.

Tena katika enzi hizo isingelikuwa vyepesi kuchukua kipande cha ardhi ya mtawala fulani na kujimilikisha k**a sehemu yako. Wateko walikuwa makini sana na wenye weredi mkubwa katika kuweka na kutunza kumbukumbu za mipaka ya eneo lao kwa kuzingatia uwenyeji katika eneo na mamlaka waliyokuwanayo ya umiliki wa ardhi.

Nadhani hata utaratibu wan chi yetu wa ardhi kumilikiwa na wananchi kwa kuiweka chini ya Raisi, ni utaratibu uliorithiwa kutoka kwa kabila la Waha. Pia ili kuhakikisha kwamba utawala unadumu na kuwa na nguvu, kulikuwa na desturi ya utawala mmoja kuvamia utawala jirani na kupigana vita. Utawala ulioonekana kushindwa katika vita hivyo ulitekwa na kutawaliwa. Hivyo tuseme kwamba tawala zote zilizokuwapo eneo lote la Buha tunaweza kusema ndizo jumla na nchi zilizokuwepo.

UTAWALA WA UJIJI;

Ujiji ni ukoo mmojawapo miongoni mwa koo nyingi za kabila la Waha. Koo hii ilikuwa moja ya Koo tawala la Wateko katika eneo la Kilemba(Mukigo). Mukigo kieneo ilijumuisha sehemu za nyakelela, NYanzali ,Kilemba na Shuza iliyopo katika bonde la mto shuza katika bonde la ufa la Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Kipindi cha ujio wa Watutsi eneo hili nalo lilikumbwa na athari ya ujio wao. Inasemekana kwamba eneo hili la Ujiji lilikuwa chini ya utawala wa HERU. Baadaye mtawala huyu aliamua kugawa sehemu ya utawala wake na kumpa mwanaye. Sehemu hii ya utawala mpya iliitwa Ujiji kutokana na jina la ukoo wa Wateko walioishi hapo. Mipaka ya eneo lake lilichua sehemu za wilaya za Kigoma vijijini, Kigoma Mjini na Uvinza.

Mtwale wa Tawala ya Ujiji wa Kilemba alipakana na Mtwale wa Tawala ya Heru kwa upande wa Mashariki aliyeishi eneo la Manyovu. Ikulu ya MWAMI WA UJIJI mwanzo ilikuwa MUKIGO, baadaye ilihamia NKALINZI/ KALINZI. Sehemu kubwa ya eneo lake lilikuwa pori na ilikuwa na wakazi wachache sana. Katika masimulizi sikupata kujua eneo lingine lililokuwa na Watwale zaidi ya Mtwale wa Kilemba.Watu waliishi katika maeneo ya Nyanda za juu tu tofauti na ilivyo sasa ambapo watu wamejaa mwambao wa ziwa Tanganyika pande za Kaskazini na Kusini. Aidha pia katika kipindi hiki hata Waarabu walikuwa bado hawajafika katika eneo la Ujiji. Kuna watu wanadhani kwamba KALINZI ni MANYOVU hapana, mwanzoni ilikuwa Manyovu chini ya Mtawala wa Heru.

Baadaye eneo la Ujiji kugawiwa kwa Mtawala mwingine ndipo jamii zilipoanza kutengana. Jamii ya Manyovu ikawa chini ya utawala wa Heru chini ya Mtwale wa Manyovu na Jamii ya Ujiji ikawa chini ya utawala wa Ujiji chini ya Mtwale wa Kilemba. Mtengano ulianzia hapo katika masuala ya kiutawala, hivyo tunaweza kusema tofauti za jamii hizi mbili zinatokana na mipaka ya utawala wakati wa Wateko na baada ya Wateko Wami.

BAADHI YA MAJINA YA WAMI WA UJIJI.

1.MWAMI RUSIMBI
2.MWAMI GWASA.
3.MWAMI George Bhatega

Address

Kigoma
Donetsk
255

Telephone

+255757668744

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NLG Motivation stories posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share