14/05/2026
Linapokuja swala la moto wa Jahanamu, bila shaka Kila mtu anaogopa maana moto unatisha.
Moto wa Jahanamu ni sehemu ya adhabu watakayoingia waovu wote hata dini 2 kubwa Duniani ukristo na Uislamu,zote zinasema waovu watatupwa ndani ya moto wa milele siku ya kiama.
Mimi k**a mchukunuzi wa mambo mbalimbali nimechukunua ndani ya biblia na Qurani π nimegundua adhabu ya moto ni Kali saana Tena saana kuliko tunavyodhania π₯Ή
Qurani na Biblia : vinazungumzia moto (adhabu) kwa lugha nzito, ya kuogofya, na yenye lengo la kuonya, kurekebisha maovu ya watu na kuhimiza toba yaani watu waache maovu wawe wema.
TUANZE NA QUR~ANI KISHA BIBLIA
1. Moto na mateso katika Qurani (Uislamu)
Katika Qurani, moto unaitwa Jahannam. Maelezo yake ni ya moja kwa moja, ya kina, na ya kutisha sana.
Maelezo ya Jahannam:
Moto unawaka milele kwa makafiri
KAFIRI : ni Kila aliefikiwa na haki akaipinga yaani mtu asiemwamini Mungu na kukataa haki na akatenda maovu mengi hapa Duniani : huyo ndie kafiri.
Ama mtu hajafikiwa na haki ,hajasikia kuhusu Uislamu alikufa bila kuskia Uislamu Wala kuujua π huyu sio kafiri na motoni haendi.
Kwa muujibu wa Uislamu Moto una viwango (ngazi) tofauti kulingana na kosa.
Ngozi huungua kisha hubadilishwa ili waonje adhabu tena.π₯Ήπ₯Ίπ³π³
Watu watanyweshwa maji ya moto yanayochemka, yanayochoma matumbo.π³π³π³
Kilio, majuto, na kuomba msaada : lakini hakuna msaada.π³π³
Aya za Qurani mfano:
βHakika wale waliokufuru ishara zetu, tutawatia katika moto; kila ngozi zao zitakapo unguzwa, tutawabadilisha ngozi nyingine ili waonje adhabu.β (Qurani 4:56)
βNa watapewa maji ya moto, yakawakatakata matumbo yao.β
(Qurani 47:15)
πLengo la maelezo haya:
Kuonya waziwazi waovu wote
Kuweka uwajibikaji binafsi
Kueleza kwamba Mungu ni Mwenye haki, si dhalimu
Lakini pia Qurani inasisitiza:
Rehema ya Mungu ni kubwa kuliko ghadhabu Yake
(mlango wa toba uko wazi hadi pumzi ya mwisho)
π Kwa waislamu mtu akifanya maovu mengi kiasi ambacho yanaweza kujaza dunia nzima ,akitubu na