11/04/2018
MAAMUZI SAHIHI NDIO CHANZO CHA MAFANIKIO NA FURAHA YA KWELI.
Wakati flani unapitia katika kipindi kigumu sana, unajikuta upo katikati ya jambo muhimu ambalo inakupasa kufanya maamuzi sahihi ili kulitatua.
Hapa nazungumzia maamuzi sahihi lakini yenye manufaa kwa wakati uliopo na hata wakati ujao.
Katika kila kitu unachotaka kufanya ni lazima ufanye uamuzi sahihi tena wenye faida.
Kumbuka yapo maamuzi sahihi lakini hayana faida, au tuseme kwa lugha nyepesi kuwa maamuzi sahihi yasiyoleta furaha ya kudumu, unaweza amua kufanya kitu ambacho kwa wakati huo uliona kina kuletea furaha lakini kumbe furaha hiyo ikawa ya kipindi kifupi tu.
Soma mfano huu.
CEO wa kampuni moja iliyokuwa na mafanikio makubwa sana alikuwa akihojiwa na mwandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kampuni ile.
Mwandish: Nini siri ya mafanikio ya kampuni yako?
CEO: akajibu kwa kifupi tu. (MAAMUZI MAZURI)
Mwandishi: akumuuliza kwa hamaki kidogo. (UNAWEZAJE KUFANYA MAAMUZI MAZURI)
CEO: Akaendelea kujibu kwa kifupi.( KUTOKANA NA UZOEFU)
Mwandishi: bila kupoteza hata sekunde akuliza ( UNAPATA WAPI UZOEFU)
CEO: huku akitabasamu.( KUTOKANA NA MAAMUZI MABAYA)
Naam mahojiano yao yalikuwa k**a hivyo.
Hapa tunapata kitu kingine kuwa ili kufanya maamuzi mazuri unahitaji uzoefu.
Lakini vile vile uzoefu tunaupata pale tunapokosea.
(TUNAJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA)
Unapokosea ni njia moja wapo ya kujifunza namna bora ya kuepuka makosa kwa wakati mwingine.
Tusiogope kukosea kwakuwa na njia mojawapo ya kujifunza ili kufanya maamuzi sahihi yenye manufaa kwetu,jamii na taifa kwa ujumla.
Mahali popote unapoona mambo hayaendi jua kabisa hakukuwa na maamuzi sahihi.
Vita katika nchi nyingi Dunia chanzo chake ni maamuzi batili
Maamuzi yanayolenga kumnufaisha mtu mmoja au upande flani huku watu wengine au upande mwingine ukiumizwa basi hakika hayo sio maamuzi sahihi.
(HAYO NI MAAMUZI YA KINYONYAJI)
Mada yetu ni ndefu sana tutaendelea nayo kadri tutakavyopata nafasi.
Lakini kuna watu wanahitaji kuwa makini kwaajili ya kufanikiwa.
Mfano.
• Wewe ambaye unafikiria kuwa ukiajiliwa ndio utapata mafanikio yako, hakikisha unafikiria vyema kabla ya kuendeleza hazma yako hiyo ili usije ukajutia hapo baadae.
• Wewe ambaye upo kwenye ajira lakini unaona kuwa ajira haikusaidii kitu na unatamani hata kuacha kazi
Tafadhari fikiria vyema na uamue kipi unataka kukifanya baada ya kuacha hiyo kazi, jitahtimini vyema hakika utafanya maamuzi sahihi.
• Wewe ambaye huna kazi wala chanzo chochote cha mapato, jipe muda zaidi wa kutafakari jiulize kwanini huna kazi wala chanzo chochote cha mapato??
Fanya maamuzi sahihi muda bado ni wako.
• Wewe ambaye unatamani kuanzisha biashara au jambo lolote lile kwaajili ya kumudu gharama za maisha
Kwanza hakikisha unapunguza mzigo mkubwa wa matamanio yako
Punguza idadi ya vitu unavyotaka kuvifanya hakikisha unabakia na jambo moja muhimu alafu anza kulifanyia tafiti ili mwishowe ulifanye kwa usahihi.
(PUNGUZA IDEA ZAKO BAKIZA MOJA TU)
• Wewe ambaye upo nyumbani tu na nyumbani kuna uwezo kiasi kwamba ufikirii maisha k**a wenzako waliopo mtaani. Hongera ila fanya maamuzi sahihi.
MAAMUZI SAHIHI NI CHANZO CHA MAFANIKIO NA FURAHA YA KUDUMU
AFRICA NA WATU WAKE. PAMOJA TUNAWEZA.