16/12/2025
KAMANDA MORCASE AHIMIZA FURSA YA VIWANJA KWA ASKARI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Salim Morcase amewaongoza Maafisa wa Polisi Mkoa wa Pwani kutembelea viwanja vya mradi wa Kampuni ya Uuzaji na Upimaji wa Viwanja ya BR Real Estate Developers Limited huko Msolwa, Chalinze, Leo Disemba 16, 2025.
Hii ni baada ya Kamanda Morcase kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa BR Real Estate Developers Limited Bw. Zeno Mboro mapema wiki hii kuhusu kupata fursa kwa maafisa, Wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kununua viwanja vya makazi au biashara katika eneo hilo la Msolwa.
Kamanda Morcase alizungumza na maafisa hao na kuwasihi waitumie fursa hiyo vizuri na yeye kwa kushirikiana na Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Pwani watawezesha mazingira rafiki kwa askari kulipa pesa hiyo ya viwanja kwa awamu.
Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo , Bw Zeno Mboro aliwapongeza maafisa waliojitokeza kuona fursa hiyo na kueleza kuwa anawakaribisha kumiliki viwanja vilivyopimwa, Kuandaliwa miundombinu ya barabara na huduma muhimu za kijamii.
Aidha, katika mradi huo wametenga eneo la Kituo cha Polisi kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi.
Kwa mawasiliano zaidi Tupigie +255 624 000 333/ +255 626 442 277 /+255 622 442 277 au tembelea Instagram brrealestateagentltd