Sifael TV

Sifael TV personal use

05/12/2022

KOCHA CHARLES BONIFACE MKWASA AJIUZULU
Kocha Mkuu wa Klabu ya Ruvu Shooting, Charles Boniface Mkwasa amejiuzulu kuifundisha timu hiyo kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza na Mtangazaji Maulid Kitenge wa EFM, Mkwasa amesema kuwa amefikia uamuzi huo ili kutoa nafasi kwa watu wengine waende wakaendeleze pale ambapo ameishia huku akiiacha timu hiyo kwenye nafasi ya 15 ya msimamo ambayo ni ya pili kutoka mwisho.
“Labda filosofi yangu imeshindwa kufanya kazi hivyo natoa fursa kwa mtu mwingine,” amesema Mkwasa.
Mkwasa na Ruvu Shooting wamecheza michezo 15 hadi sasa, ushindi mara tatu, sare mbili na wamepoteza michezo kumi ambayo ni mingi kulinganisha na timu yao ya msimu uliopita.
Mzunguko wa kwanza umeisha wakiwa katika nafasi mbaya, wakiwa wamepoteza mechi mechi nne mfululizo mpaka sasa huku mara yao ya mwisho kupata ushindi ilikuwa ni Septemba 29 na sasa ni Desemba.
Mechi inayofuata watamenyana dhidi ya Ihefu ambao nao wanajikongoja kujinasua kutoka chini kwenye msimamo wasije angukia play offs au kushuka daraja tena.
Hivyo timu hiyo sasa haina kocha.

03/10/2022

UNAODAIWA NI WARAKA WA KATIBU WA MASANJA
Katibu wa Kanisa la Feel Free Church linalomilikiwa na mchekesahaji Masanja Mkandamizaji anadaiwa kujiua kwa kujinyonga kisha kusambaa kwa waraka unaodaiwa kuachwa na katibu huyo k**a ifuatavyo;
“Ujumbe wangu wa mwisho kwako Monica. Asante kwa kunipenda kipindi chote hakika umenipa upendo ambao umeacha alama moyoni mwangu ambao kila nikijaribu kuifuta nimeshindwa sioni upendo wako wa mwanzo hivyo nimebaki kuumia moyoni kwa kukosa REAL LOVE FROM YOU.
Monica ulinipenda sana na kuniahidi kutoniacha siku zote na ahadi zako nilizipokea moyoni nami kukuahidi kukupenda sana na hii ndo inaniumiza sana Monica. Asante kwa penzi lako ambalo halijawahi kutoka moyoni mwangu sioni tena haja ya kuishi kwenye hii dunia.
Bila penzi lako nasema siwezi Monica samahani kwa maamuzi nitakayoyafanya najua huamini k**a naweza kufanya hivi kwa sababu ya penzi lako but naomba upelewe kua umefanya nione thamani ya mapenzi katika huu ulimwengu kupitia wewe so siwezi kuishi bila penzi lako.
Sioni tena maana ya maisha. Monica, inawezekana huu ni ujumbe wangu wa mwisho kwako pia acha dunia nzima itambue kuwa nakupenda sana Monica na nimeshindwa kuishi bila wewe.
Najua familia yangu, marafiki zangu na mama yangu mzazi utaumia juu ya hili, lakini nisamehe sana mama yangu. Najua unanipenda na mimi nakupenda mama.
Monica nakupenda sana and I’ll miss you so much. Your love, your time and your moment bye kiosho.
Kuliko ukaona ujumbe huu kwenye mitandao ya kijamii bora nikutumie wewe, ujue yaliyo moyoni mwangu na ukiweza kunitibu kwa ule upendo wako wa kwanza nitakua mzima ila ukipuuzia hii basi utanipoteza na huu ndiyo utakuwa ujumbe wa mwisho kwangu.

03/10/2022

MASANJA AFUNGUKA, ASEMA HILI LITAPITA, AOMBA TUMUOMBEE
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mchekeshaji na Mchungaji Masanja Mkandamizaji ameposti picha akiwa na mkewe Monica wakimuomba Mungu na kusema;
“Kila kazi ina gharama yake!! Acha tulipe gharama ya tulichoitiwa. Nakupenda mpaka pumzi yangu ya mwisho mke wangu. Hili nalo litapita…
Tuombeeni nasi tunaomba.
Mtetezi wetu yu hai…”

10/09/2022

SIMBA KUVAANA NA NYASA BIG BULLETS
Klabu ya Simba leo inashuka dimbani kuvaana na Nyasa Big Bullets ya Malawi katika Uwanja wa Taifa wa Malawi wa Bingu wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 41,100.
Hii ni mechi ngumu kwa Simba kwa kuwa mara nyingi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mcheza kwao hutunzwa.
Big Bullets ambao msimu uliopita kwenye mashindano hayo walitolewa hatua ya kwanza wanajivunia safu yao ya ushambuliaji ambayo imekuwa na uwezo wa kufunga mabao mengi kila mara inapopata nafasi.
Mshindi wa jumla wa mechi hiyo atacheza na mshindi wa mchezo kati ya Red Arrows ya Zambia au Agusto ya Angola.
Cc;

09/09/2022

RASMI RAYVANNY NA FAHYMA WAMERUDIANA
Awali kulikuwa na tetesi nyingi kuwa, msanii Rayvanny amerudiana na mpenzi wake, mrembo Paula Kajala, lakini kumbe mambo yalikuwa ni tofauti kwani aliyerudiwa ni Fahyma; baby mama wa jamaa huyo.
Hii ni baada ya Rayvanny kumposti Fahyma kwenye Snapchat, jambo ambalo hajalifanya yapata miaka miwili sasa.
Kitendo hicho kimemuibua Paula ambaye kwa sasa anarusha vijembe kwa Rayvanny huku akimsifia Harmonize ambaye ni mchumba wa mama yake, Kajala Masanja.
Katika moja ya posti zake, Paula anaimba wimbo wa Harmonize wa Bakheresa akiwaponda wanaume ambao ni bahili huku akimsifia Harmonize kwa kuweza kumuhonga mama yake magari mawili ya kifahari aina ya Range Rover zenye majina ya Kajala 1 na Kajala 2.
Wengi wanaamini hilo ni dongo kwa Rayvanny ambaye inasemekana ni bahili wa kutupwa kwani alishindwa kumfanyia Paula makubwa ikiwemo kumfungulia duka la nguo, jambo ambalo Harmonize amelifanikisha.
Sasa; k**a kawaida yake, Fahyma ameanza kutamba kwamba yeye ni mwanamke mzuri sana na haiwezekani mwanaume akamuacha na akifanya hivyo, atarudi tu@
Cc;

09/09/2022

MBOSSO: RAYVANNY LAZIMA TUFANYE KAZI
Mwimbaji mkali wa Bongo Fleva, Mbosso Khan anasema kuwa, licha ya msanii mwenzake, Rayvanny kuondoka kwenye Lebo ya WCB, bado wanaweza kufanya kazi pamoja kwa kuwa ni marafiki na mara kwa mara wamekuwa wakionana.
Julai, mwaka huu, Rayvanny aliiaga rasmi WCB aliyoitumikia kwa miaka sita na kwa mafanikio makubwa na sasa amejikita katika lebo yake ya Next Level Music ambayo inamsimamia msanii Mac Voice.
“Ni mwanangu, kwa hiyo inapokuja kazi ambayo natakiwa nifanye na Rayvanny lazima tufanye ni rafiki yangu, nakutana naye, anakuja ofisini tunapiga stori, yaani hakuna noma,” anasema Mbosso.
Chini ya WCB, Mbosso alimshirikisha Rayvanny katika wimbo wake uitwao Pakua kutoka kwenye albam yake ya Definition of Love huku Rayvanny akimshirikisha Mbosso kwenye ngoma yake ya Zuena inayopatika kwenye albam yake ya Sound From Afrrica.
Cc;

09/09/2022

MCHUNGAJI ACHARUKA VIJANA KUOA/KUOLEWA NA WAZEE
Mchungaji maarufu nchini Tanzania, Daniel Mgogo amecharukia suala la vijana wadogo kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na wazee waliowazidi umri maradufu.
Mchungaji Mgogo amewazomea vijana hao na kuwataka kujiepusha na mitego k**a hiyo kwani tabia hiyo ni k**a kushiriki katika kula mali ya babu yako aliyetangulia mbele ya haki kitambo.
Mgogo pia hakuwasaza wakongwe hao wanaojiingiza katika mapenzi ya vijana wadogo, wake kwa waume akiwataka kujiheshimu na kukoma kuwapotosha vijana kwani kanisa linataka vijana wengi kufanya harusi na vijana wenzao ili kukuza kizazi kijacho.
Mgogo akionesha kuchukizwa, alipinga vikali dhana kwamba umri ni namba tu na kusema kwamab hakuna vile vijana wanaweza ingia katika mapenzi na wazee na mahusiano hayo kutarajia kupata watoto wa kuendeleza kizazi cha usoni.
“Kijana mbichi anajihusisha kimapenzi na jimama. Baba zake walijishughulisha naye ana hili baba zake walizaa watoto na huyu mama na wewe unaenda, utazaa watoto na huyu ana miaka sabini. Alafu mnatuambia, umri namba. Vijana tunategemea waoe tufunge harusi, watuletee wajukuu. Watu wanasukumana na mabibi minyanya,” Mchungaji Mgogo alitema moto.
Anawakashfu vijana wengi siku hizi ambao wanatebwereka na kusubiria embe kudondoka kutoka mtini pasi na kufanya juhudi zozote za kukwea ili kulichuma lile embe kwa nguvu zao.
Kwa mujibu wa Mgogo, vijana hao wanafanya kula mali za babu zao jambo ambalo amechukizwa nalo.
“Kweli kijana mdogo jitegemea, unataka kula mali za babu yako aliyekufa alimuacha huyu bibi. Wachana na huyo mama! Nenda tafuta size yako tunataka watoto,” Mgogo anasisitiza.
Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na matukio yasiyo ya kawaida ambapo unawapata vijana wadogo wanajihusisha katika mahusiano ya kimapenzi na ajuza na babu waliopitwa na umri na unapata baadhi ya watu wanashabikia mahusiano hayo, jambo ambalo kwa mchunaji Mgogo si kitu cha kufurahisha bali kukemewa vikali kwa sababu wengi wakilikumbatia, basi kizazi cha kesho hakimo.
Cc;

09/09/2022

NIKIFA KIBA ASIFIKE KWA MSIBA WANGU
Issa Azam; ni ndugu wa msanii King Kiba ambaye alifanya kufuru ya karne kumtenga nduguye na kuungana na hasimu wake, Diamond Platnumz na sasa ameibuka na mapya tena.
Issa mwenye ukaribu na msanii Diamond Platnumz wengi wanamjua k**a chawa wa WCB.
Issa mwenyewe mara kadhaa amekuwa akiliweka wazi suala hilo ikiwemo mshahara anaoupata kutoka kwa Diamond Platnumz kwa kazi yake ya uchawa.
Issa kwa kuwakomesha wanaomsema vibaya Simba, mshahara wake alisema ni mnono mno kwa mwezi.
Issa anasema kwamba mshahara wake kutoka kwa Diamond ni mara nne zaidi ya Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Mimi mshahara yangu nikiungaunga, ni mishahara minne ya Mbunge,” anasema Issa.
Issa anaonesha chuki yake dhidi ya King Kiba na wanafamilia wengine kwa kile anachosema kwamba aliwachukia kwa kutaka kumuua Diamond kwa kumpiga mawe ila wakashindwa.
Issa anaweka wazi kwa mara nyingine tena kwamba ikitokea amefariki leo hii, basi watu wa familia ya King Kiba wasijaribu kufika kwenye msiba wake kumzika.
“Mimi leo hii nikifa, kwenye kaburi langu nisiwahi waona watu hao. Msiba wangu utasimamiwa na watu wa Wasafi. Msimamizi wa msiba wangu atakuwa Nasibu Abdul (Diamond Platnumz). Naomba Diamond anizike ili nife kwa furaha. Kiba asifike kabisa kwenye msiba wangu, hata kwangu asijaribu kufika,” anasema Issa.
Cc;

08/09/2022

MCHUNGAJI AWATANDIKA VIBOKO WAUMINI
Wengi wanasema katika usasa huu wa utandawazi, ni vigumu kuficha maovu kwani kwa urahisi wa kamera, yanasambaa haraka.
Nchini Uganda mchungaji mmoja amejikuta matatani baada ya video kusambaa ikimuonesha akiwapa baraka waumini kanisani kwa njia ya kuwatandika viboko.
Mchungaji huyo alinaswa kwenye kamera akiwapiga viboko waumini kanisani; wake kwa waume, wadogo kwa wakubwa huku akidai kwamba ni moja kati ya njia za kuwamiminia baraka na upako utokao kwa Mungu.
Katika video hiyo, mchungaji huyo aliyetambulika kwa jina Nabii Kevin Kintu anaonekana akiwaombea wafuasi wake alipowaomba waje kupokea fimbo hiyo ikiwa ni sehemu ya maombi hayo. Wafuasi walianza kukusanyika mbele ya kanisa, ambapo walipigwa migongo na makalio.
Video hiyo haikuwafurahisha wengi kwani wanakashfu kitendo hicho, hasa pale ambapo Nabii Kintu alikuwa habagui mtu hata mmoja mpaka wazee wa umri uliopitiliza ambao walilazimika kukubali baraka za nabii.
Wengine wanasema kwamba adhabu ya kuchapwa viboko ilihama shuleni na sasa imekita mizizi makanisani ambapo waumini wote wanakipata cha mtema kuni wakiamini ni baraka na upako.
Cc; Sifael Paul

Address

Dar Es Salaam
DAR

Telephone

+255713750910

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sifael TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share