Huduma Ya Vitabu Vya Kiroho

Huduma Ya Vitabu Vya Kiroho Jipatie vitabu vya kukujenga ,kukuimarisha na kukuongeza katika maisha ya kiroho, Uongozi, Ushauri, na Huduma.

Uamsho wa Roho Mtakatifu1.Kazi isiyo ya kawaida ya Roho Mtakatifu inayoleta Matokeo yasiyo ya kawaida kwa kanisa.2. Uams...
04/11/2024

Uamsho wa Roho Mtakatifu

1.Kazi isiyo ya kawaida ya Roho Mtakatifu inayoleta Matokeo yasiyo ya kawaida kwa kanisa.

2. Uamsho unarejea kwenye kuamka kiroho kutoka katika hali ya usingizi au kudumaa ya maisha ya mwamini. Hujumuisha uwekwaji upya wa upendo wa Mungu, kuthamini utakatifu wa Mungu, na shauku ya Neno lake na Kanisa lake. Uamsho unaleta ufahamu wenye usadikisho wa dhambi ya kibinafsi na za pamoja, roho ya unyekevu na hamu ya kutubu na kukua katika haki.

3.Waefeso 5: 14
Hivyo husema, Amka wewe usizianye, Ufufuke katika Wafu, Na Kristo atakuangazia.

4.Uamsho unaanzishwa kwa msukumo wa Roho Mtakatifu, akiumba utambuzi wa kuhisi na kuona wa kitu fulani kinakosekana au hakipo sawa katika maisha ya mwamini ambacho tu kinaweza kufanywa sawa na Mungu.

5.“Uamsho unaanza na watu wake Mungu mwenyewe. Roho Mtakatifu anagusa mioyo yao kwa upya, na anawapa kibali kipya, mzigo mpya na shauku mpya, na mwanga mpya na maisha mpya …”

6.Mungu anapotaka kutuma uamsho huwa ana anza na watu wake, ana wachukua kando, na kuwa weka kipande kwa kipande na kisha ana warudishia tena pamoja kuwa aina ya watu anaowataka kuwa. Kile ambacho kila mtu wa Mungu anahitaji ni uamsho binafasi, uamsho unapaswa kuwa ni wa kibinafsi na wakivitendo, kabla haujawa ni wa pamoja na wa jumla.

7.Tukitaka kuona uamsho ni lazima tuache shughuli zetu. Kanisa tumetingwa mno na shughuli, kiasi kwamba hatuna muda wa kumtafuta Bwana. Tupo “busy” mno na kazi ya Bwana na hatuna muda na Bwana mwenye kazi.

8.Hakuna uamsho mkuu ulioanza bila ya toba na kuungama. Uamsho ni lazima uanze na watu wa Mungu na uanze ndani ya kanisa. K**a tunataka kuona uamsho kuna jambo moja rahisi, “Tumrudie Mungu”

9.Hakuna Uamsho bila ya toba, Toba ndio fundisho kuu la uamsho wa kiroho. Masharti muhimu ya uamsho ni kwamba, Neno la Mungu lazima lihubiriwe na viwango vitakatifu vya Mungu lazima vijulikane kwa watu. Ni lazima kuwe na kuona hatia na kuthibitishiwa kuhusu dhambi.

10.Ufunuo 2:4- 5
Lakini Nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo
wako wa kwanza. Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.

Kina patikana .
16/10/2024

Kina patikana .

11/09/2024

Amani ya Mungu italinda mioyo yetu na akili zetu wakati wa shida. Ni amani tofauti na chochote ambacho ulimwengu unaweza kutoa na ni dawa ya hofu na wasiwasi.
Wafilipi 4:7

11/09/2024

Tunapojifunza kutegemea Roho Mtakatifu na kuelewa kwamba atakuwa pamoja nasi katika hali yoyote, tutakuwa na utulivu zaidi na wasiwasi utakuwa mbali zaidi.

11/09/2024

Amani ni kukaa kwa raha na kujua kwamba Mungu yuko karibu na upande wako bila kujali nini. ... tunapokuwa na Roho Mtakatifu ndani yetu na kati yetu, tunaweza kukaa kwa amani.

17/08/2024
27/07/2024

Kila Mtu ana muda wa kusoma BIBLIA angalau dakika 10 kila siku. Ukisema huwezi tenga dakika 10 tu basi suala hapo sio kutokuwa na muda, Bali ni kutokuwa na Hamu ya Kusoma BIBLIA.

                                                                                       Katika Mtazamo Wa Kibiblia Na Kis...
03/07/2024

Katika Mtazamo Wa Kibiblia Na Kisaikolojia

Afya ya akili ni mada tata ambayo imekuwa ni changamoto inayo athiri watu wengi kwenye nyanja zote za maisha. Leo hii matatizo ya afya ya akili na magonjwa ya akili yanayo ongezeka sana na kuwa ni kawaida katika jamii. Ni uhalisia wa kweli kwamba mtu yeyote yule anaweza kupitia changamoto na mapambano ya afya ya akili. Ili kuepukana na mtazamo potofu unaozunguka masuala ya afya ya akili katika jamii, tunahitaji kuweka kipaumbele katika elimu na ulewa sahihi kwa kujielemisha wenyewe na wengine juu ya uhalisia wa changamoto za afya ya akili, magonjwa ya akili, matibabu mbadala yaliyopo na athari ambazo zinaweza kuwepo juu ya maisha ya watu.

Kujali afya zetu za akili ni muhimu sana kwa sababu afya ya akili inashawishi na kuathiri sehemu nyingine nyingi za maisha ya mtu ya siku kwa siku kuanzia vile anavyofikiria, anavyohisia, anavyotenda na anavyoweza kukabiliana na hali k**a wasiwasi, hofu, msongo, mfadhaiko, majeraha na maumivu ya kihisia, kuvunjika moyo, huzuni na mengine k**a hayo.

Pamoja na kwamba afya ya akili ni mada changamano na tata bado kuna tumaini na uponyaji unaopatikana kupitia sala na maombi, imani katika Neno la Mungu na katika matibabu ya kitaalamu. Kwa kutumia kanuni za kibiblia katika maisha yetu na kupata msaada wa kisaikolojia tunaweza kustawisha afya zetu za akili na kuwa na uthabiti na amani.

Kitabu hiki kimeandikwa kwa mtazamo wa kibiblia na kisaikolojia na utapata fursa ya kujifunza mambo mengi kuhusu afya ya akili na hisia, k**a vile, uhusiano wa afya ya akili na afya ya mwili, sababu na vyanzo za matatizo ya afya ya akili, dalili mbalimbali za matatizo ya afya ya akili, aina za magonjwa ya akili, kinga na tiba dhidi ya matatizo ya afya ya akili na jinsi ya kuwapa huduma ya kwanza ya ushauri wale wanaopitia changamoto ya afya ya akili.

Meinrald A. Mtitu

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Huduma Ya Vitabu Vya Kiroho posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Huduma Ya Vitabu Vya Kiroho:

Shortcuts

Share