The Balm Bookshop

The Balm Bookshop Books, Publishing, Christian Materials
Vitabu, Uchapaji, Bidhaa za Kikristo...πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

Kila Mwamini Ana Imani.Huwezi kwa namna yoyote kuzungumzia somo la Imani pasipo kuingia katika sura ya 11 ya Marko, kwa ...
11/08/2025

Kila Mwamini Ana Imani.

Huwezi kwa namna yoyote kuzungumzia somo la Imani pasipo kuingia katika sura ya 11 ya Marko, kwa sababu katika kifungu hiki cha andiko ndiko kauli za kushangaza, na kusisimua, kauli nzuri ajabu juu ya somo la Imani zilipata kunenwa kutoka kinywani mwa Bwana.
MARKO 11:22-26
Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu.
Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
Lakini k**a ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]

Nilichofanya katika kitabu hiki ni kuweka majumuisho ya vitu saba muhimu kuhusu somo la Imani. Na ukweli wa kwanza muhimu kuhusu Imani ni: kila mwamini ana kiasi fulani cha aina ya Imani-ya kiungu.
Nilizoea kufanya mikutano ya muda mrefu. Kwa miaka mingi sikukubali mwaliko wowote chini ya majuma matatu. Tungefanya mikutano kwa makanisa mitaani, na wakati mwingine tuliweka mikutano yetu wenyewe.
Katika siku hizo, nisingekubali mwaliko chini ya majuma matatu. Na mara nyingi tulikaa sehemu moja kwa majuma manne hadi nane. Wakati mmoja tulikaa majuma tisa. Tulifanya ibada mbili kwa siku, siku tano kwa wiki.
Ndiyo, tulipokaa muda mrefu hivyo β€” hasa majuma manne hadi tisa β€” tulikuwa na muda wa kutosha kuangalia kila kitu kinachohusu somo la Imani na kupindua kila jiwe na kukagua kila mwamba. Kwa mfano, tulizungumzia vitu k**a, Ikiwa Imani yako haifanyi kazi, ni kwanini haifanyi kazi? Tungelishughulikia hili na maeneo mengine ya Imani, na tuliita hiyo "Kliniki ya Imani."

Lakini unapokuwa katika mkutano na watu kwa muda wa wiki moja tu, na una ibada tano au sita tu, unalazimika kuminya somo lako na kuwapa kwa namna ya dozi. Kwa maneno mengine, unawapa tu yale yaliyo ya msingi katika somo la Imani, yaliyobaki unayaacha.
Hivyo katika kitabu hiki, nitakuongoza katika uelekeo sahihi. Halafu utaendelea mwenyewe kujifunza mengine juu ya imani.
Zingatia Marko 11:22 ya andiko letu: "Yesu akajibu akamwambia, Mwaminini Mungu." Maelezo ya tafsiri ya Bibllia ya Mfalme James yanasoma kwamba Yesu alisema, ". . . Iweni na imani ya Mungu."
Tafsiri nyingine inasoma (kwa kweli, Wasomi wa Kigiriki wanatuambia ndio tafsiri yake Orijino): "Iweni na imani ya Mungu." Kwa ufasaha kabisa, Yesu alisema, "Iweni na Imani ya Mungu!"

-Kenneth E. Hagin.

Sifa za Upendo wa Ki-MunguBasi, sasa inadumu Imani, tumaini, upendo, haya matatu; NA KATIKA HAYO LILILO KUU NI UPENDO. β€”...
11/08/2025

Sifa za Upendo wa Ki-Mungu

Basi, sasa inadumu Imani, tumaini, upendo, haya matatu; NA KATIKA HAYO LILILO KUU NI UPENDO.
β€” 1 Wakorintho 13:13
Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, KWA MAANA MUNGU NI UPENDO.
β€” 1 Yohana 4:8
Biblia inasema kuwa Mungu ni upendo. Vilevile husema kuwa upendo ni mkuu kuliko Imani au tumaini. Sawa, kwa kuwa Mungu ni upendo, basi tunahitaji kujua upendo ni nini β€” yaani, aina ile ya upendo alionao Mungu.
Katika Wakorintho wa Kwanza 13:13, toleo la biblia ya Mfalme James linatafsiri neno "upendo" k**a hisani. Kwa kweli, inasikitisha kwamba neno "agape" lilitafsiriwa k**a hisani, kwa sababu tafsiri hiyo haifafanui vizuri maana kamili ya neno la Kigiriki lililotumika katika mstari huu.

Kulingana na kamusi, neno "hisani" linamaanisha nia njema ya ukarimu au upendo wa ubinadamu. Lakini neno lenyewe la Kigiriki linalotumiwa hapa ni "agape," linalomaanisha upendo wa Ki-Mungu. Mahali pengine katika Agano Jipya, neno "agape" linatafsiriwa upendo badala ya hisani.
Kwa mfano, katika Yohana wa Kwanza 4:8, biblia inasema wazi, "Mungu ni agape." Kwa maneno mengine, Mungu ni upendo. Hivyo neno "agape" linamaanisha aina ya upendo alionao Mungu.

Agape au upendo wa Ki-Mungu ni nini? Kabla sijajibu hilo, hebu nikuonyeshe kitu cha kushangaza kuhusu upendo wa Mungu. Biblia inasema kuwa upendo ni mkuu kuliko tumaini au imani (1 Kor. 13:13). Kwanini upendo wa Ki-Mungu ni mkuu kuliko tumaini au imani?
Kwanza kabisa, Imani haitafanya kazi pasipo upendo. Kwa maneno mengine, Imani inategemea Upendo ili ifanye kazi. Wagalatia 5:6 inasema, "Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo."
Unaweza kuona dhahiri kwamba upendo utatakiwa kuwa mkuu au mkubwa ikiwa Imani haiwezi kufanya kazi pasipo huo. inagharimu upendo kuifanya Imani itende kazi.
Pili, Imani haitafanya kazi pasipo tumaini. Tafsiri ya Kiingereza cha Kisasa katika Waebrania 11:1 inasema, "Imani huleta uhalisia kwa matumaini yetu." Unahitajika kutarajia kitu fulani kabla ya Imani yako kukipa uhalisia kitu hicho. Hivyo Imani pia hutegemea tumaini.

WAEBRANIA 11:1
Basi IMANI ni kuwa na hakika ya mambo YATARAJIWAYO (TUMAINI), ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Unaona, usipotaraji chochote, Imani yako haiwezi kufanya kazi kwa sababu haina shabaha au kitu cha kumwamini Mungu kwacho. Kwahiyo, Imani haiwezi kufanya kazi pasipo tumaini. Vilevile, Imani inategemea upendo ili ifanye kazi. Ndio sababu biblia inasema kuwa upendo ni mkuu kuliko tumaini na imani (1 Kor. 13:13).

1 WAKORINTHO 13:1-3
Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, k**a sina upendo [Aina ya upendo alionao Mungu], nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, k**a sina upendo [Aina ya upendo alionao Mungu], si kitu mimi.
Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, k**a sina upendo [Aina ya upendo alionao Mungu], hainifaidii kitu.

Biblia husema kuwa hata k**a karama zote za Roho zikidhihirishwa kupitia sisi, pasipo upendo wa Mungu, haitatufaidia kitu! Itakuwa bure kabisa. Fikiri kuhusu hilo!

K**a tukifahamu siri zote na kuwa na maarifa yote na Imani timilifu, lakini hatuna upendo wa Mungu ukifanya kazi ndani yetu, ukitiririka kupitia sisi, haitatufaa chochote! Hata kutoa kwa maskini na kujitoa dhabihu si kitu isipokuwa tumesukumwa na upendo.

Hakuna unachofanya kitakachokupa faida isipokuwa kimefanywa kwa msukumo wa upendo wa Mungu. Unaweza kuona dhahiri kwanini aina ya upendo alionao Mungu ni muhimu sana na kwanini biblia inasema ni mkuu kuliko Imani na tumaini.
Vilevile, biblia inasema kuwa ni kupitia upendo β€” upendo wa Mungu ndani yetu β€” kwamba watu wote watatambua kuwa sisi ni wanafunzi wake. Biblia haikusema ni kwa Imani au tumaini kwamba watu wote watatambua tu wanafunzi wake. Hapana, ni kupitia upendo wa Mungu ukidhihirishwa ndani yetu na kupitia sisi ndipo watu wote watatambua sisi ni Wakristo.

YOHANA 13:35
Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, MKIWA NA UPENDO NINYI KWA NINYI.

Ulimwengu utajuaje kuwa sisi ni Wakristo? Kwa sababu twapendana sisi kwa sisi.

Na kwa kuwa upendo wa Mungu uko ndani yako, basi waweza kuchukuliana na yote yanayojitokeza. Labda ulisema, "Siwezi kuvumilia zaidi ya hapa." Au "Siwezi kuchukuliana na Fulani na Fulani zaidi ya hapa." Lakini upendo wa Mungu ukifanya kazi ndani yako na kupitia wewe hakika unaweza!

- Kenneth E. Hagin.

Tunaishi katika siku ambayo hatuna muda wa kucheza kanisani au kuleta mzaha na michezo ya ibilisi katika maisha yetu. Si...
11/08/2025

Tunaishi katika siku ambayo hatuna muda wa kucheza kanisani au kuleta mzaha na michezo ya ibilisi katika maisha yetu. Siku za mwisho ziko juu yetu. Mwisho wa mambo yote umekaribia. Miaka ya hatari iko mbele yetu, kwa sababu kuna kazi kubwa ya kufanya na mavuno makuu ya nafsi kuvunwa.

Kamwe haijawahi kuwa muhimu kwetu kiasi hiki kwamba tuwe huru mbali na yote yaliyotufunga huko nyuma. Kamwe haijawahi kuwa muhimu kwetu kwamba tuwe wasikivu kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu na kwa kila mmoja wetu kufuata mpango wa Mungu kwa maisha yetu. Rafiki! Ni wakati wa kukaa sawa. Ni wakati wa kumaanisha kuhusu kumtumikia Mungu na kuwa vyote ambavyo Mungu anatutaka tuwe.

Unapotembea katika utii kwa Mungu, kushindwa kwako kulikopita na makosa yaliyokuzuia kutembea katika Roho hayataweza kuzuia yale Mungu amekukusudia kutimilizwa. Ikiwa utafanya sehemu yako kwa kujiandaa na kutii, mipango yote ya kimwili ya mwanadamu na mapepo yote kuzimu hayataweza kuzuia mpango wake kutimilizwa. Hakuna kitakachoweza kuondoa au kufuta kile Mungu ametangaza kwa maisha yako!

β€œMaana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.
Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote..”

β€” Yeremia 29:11-13

Eeh Bwana, kile nisichokiona, nionyeshe wewe.

Kile nisichokijua, nifundishe wewe.

Na kwa kile ulichoniandalia, niandae kwacho.

- Kenneth E. Hagin.

Kila mtu alikuwa akiomba madhabahuni, na nikapiga magoti jukwaani nyuma ya kiti cha kukunja karibu na madhabahu. Nikaanz...
11/08/2025

Kila mtu alikuwa akiomba madhabahuni, na nikapiga magoti jukwaani nyuma ya kiti cha kukunja karibu na madhabahu. Nikaanza kunena kwa lugha, na nikasikia sauti ikisema, "Njoo huku juu." Mwanzoni, sikutambua kwamba sauti hiyo ilikuwa ikisema nami. Nilidhani kila mtu aliisikia.
"Njoo huku juu," sauti ilisema tena. Basi nikainua macho na kumwona Yesu amesimama juu ya kilele cha hema. Nilipotazama tena, hema lilikuwa halipo, viti vya kukunja vilikuwa havipo, kila nguzo ya hema ilikuwa haipo, madhabahu ilikuwa haipo, na Mungu aliniruhusu kuona katika ulimwengu wa roho.

Yesu alikuwa amesimama hapo, nami nikasimama Uweponi Mwake. Alikuwa ameshika Taji Mikononi mwake. Taji hii ilikuwa nzuri kupita kiasi, hakuna lugha ya kibinadamu ya kuielezea. Yesu akaniambia, "Hii ni Taji ya Mvuna Nafsi. Watu wangu ni wazembe na wabishi. Taji hii ni kwa ajili ya kila Mtoto wangu. Nazungumza na Kusema, 'Nenda ongea na yule au mwombee fulani,' lakini watu wangu wametingwa sana. Wanapuuza, na nafsi zinapotea kwa sababu Hawataki Kunitii." Yesu aliposema hivyo, nililia mbele zake. Nilipiga magoti na kutubu kushindwa kwangu.

Kisha Yesu akaniambia tena, "Njoo huku juu." Ilionekana k**a nilienda pamoja naye kupita anga mpaka tukaufikia mji mzuri. Hatukuingia ndani ya mji huo, lakini tuliutazama kwa karibu k**a ambavyo mtu anaweza kwenda juu mlimani na kutazama chini bondeni. Uzuri wake ulikuwa zaidi ya maelezo! Yesu akasema kwamba watu kwa ubinafsi wanasema kwamba wako tayari kwenda mbinguni. Wanaongea kuhusu majumba yao na utukufu wa Mbinguni ilhali wengi wao wanaishi katika giza na kukata tamaa. Yesu akaniambia niwashirikishe tumaini langu na kuwaalika kuja Mbinguni pamoja nami. Kisha Yesu alinigeukia na kusema, "Sasa hebu twende kuzimu."

Tulishuka chini kutoka Mbinguni, na tulipofika duniani hatukusimama, bali tuliendelea kwenda. Maandiko mengi katika biblia yanaonyesha kuzimu kuwa chini yetu. Kwa mfano, "Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, ili kukulaki utakapokuja. . . utashushwa mpaka kuzimu; mpaka pande za mwisho za shimo.." (Isa. 14:9,15). Isa. 14:9,15). "Kwahiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake. . .naye pia. . .hushuka na kuingia humo" (Isa. 5:14).
Tulishuka chini kuzimu, na tulipofika mahali hapo, niliona kile kilichoonekana k**a wanadamu wakiwa wamefunikwa kwa miale ya moto. Nikasema, "Bwana, hii inaonekana k**a wakati ule nilipokufa na kuja mahali hapa Aprili 22, 1933. Uliongea, na nikarudi duniani kutoka mahali hapa. Na kisha nikatubu na kuomba, nikatafuta msamaha Wako, na ukaniokoka. Isipokuwa sasa najisikia tofauti: Sasa siogopi wala kutishwa, k**a nilivyokuwa zamani."

Yesu akaniambia, "Waonye watu, wanaume kwa wanawake kuhusu mahali hapa," na kwa machozi, nikalia kwamba nitawaonya.
Kisha akanirudisha duniani. Nikajitambua kwamba nilikuwa nimepiga magoti jukwaani kwenye kiti cha kukunja na Yesu alikuwa amesimama pembeni yangu. Akiwa amesimama hapo, aliongea nami kuhusu huduma yangu. Aliniambia baadhi ya mambo kwa ujumla ambayo baadaye aliyafafanua kwa ufasaha katika maono mengine. Kisha Yesu akatoweka, na nikagundua nilikuwa bado nimepiga magoti jukwaani. Niliweza kuwasikia watu wakiomba kunizunguka.

Nilipoanza huduma miaka 49 iliyopita, natamani tungekuwa na nyenzo zinazopatikana leo. Huduma na maisha yetu yangekuwa t...
11/08/2025

Nilipoanza huduma miaka 49 iliyopita, natamani tungekuwa na nyenzo zinazopatikana leo. Huduma na maisha yetu yangekuwa tofauti.
Ndio sababu nataka kuwashirikisha wahudumu wengine β€” hasa wahudumu vijana β€” kile kilichotuchukua baadhi yetu miaka 40 au 50 kujifunza.
Katika kitabu hiki nataka kujadili kile nilichojifunza kuhusu upako takribani nusu karne ya huduma yangu. Kuna mengi mno katika roho yangu ya kuwashirikisha.

Katika sehemu ya 1, tutajadili upako wa mtu mmoja mmoja ambao kila mwamini anao katika Kuzaliwa Upya. Tutaweka wazi kwamba waamini wote wanaweza kuwa na upako wa kina zaidi kwa kubatizwa na Roho Mtakatifu. Uzoefu huu ulio wazi kwa waamini wote, ni kwa ajili ya utumishi.

Sehemu ya 2 tutaona kwamba upo pia upako wa Roho Mtakatifu katika vipawa vya huduma β€” upako unaoenda pamoja na ofisi.
Ashukuriwe Mungu kwa ajili ya karama za huduma alizoziweka katika mwili wa Kristo ili tuweze kukua. Ashurukiwe Mungu kwa ajili ya upako wa Mungu juu ya Wanaume na Wanawake aliowaita katika huduma za ofisi hizi.
Hata bado kuna upako ulio imara zaidi, upako wa pamoja, ambao uko juu ya kanisa. Tutajifunza upako huu katika sehemu ya 3.
Weka akilini unaposoma kitabu hiki kwamba hizi ni aina mbalimbali za upako, lakini zote ni kutoka kwa Roho Mtakatifu mmoja β€” mshirika pekee katika Uungu afanyaye kazi duniani leo.
Utagundua kwamba hakuna kilicho zaidi ya utukufu wa Mungu unapodhihirika. Mara utakapo uonja, hakuna kingine kitakutosheleza.

- Kenneth E. Hagin
Tulsa, Oklahoma. Julai 1983.

Mungu amekuwa akizungumza nami hivi karibuni kuhusu kitu fulani ambacho nilifeli kukifanya.Miaka ishirini iliyopita, mwe...
11/08/2025

Mungu amekuwa akizungumza nami hivi karibuni kuhusu kitu fulani ambacho nilifeli kukifanya.

Miaka ishirini iliyopita, mwezi Februari mwaka 1959 mjini El Paso, Texas, Bwana alinitokea katika maono. Aliingia chumbani mwangu saa 6:30 wakati wa mchana, akaketi kwenye kiti pembeni ya kitanda changu, na akaongea nami kwa takribani saa moja na nusu. Naeleza zaidi kuhusu hili ndani ya kitabu hiki, lakini nataka kusisitiza hapa kitu fulani kwanza.

Akaongea nami kuhusu huduma ya nabii (Efe. 4:11,12). Kisha akasema, "Sikuwaweka manabii katika Kanisa ili waliongoze Kanisa la Agano Jipya. Neno Langu linasema, 'Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.' Sasa ikiwa utanisikiliza, ninaenda kukufundisha jinsi ya kumfuata Roho wangu. Halafu, nataka wewe uwafundishe watu wangu jinsi ya kuongozwa na Roho."

Naona aibu kwamba nimeacha miaka ishirini kupita pasipo kufundisha vya kutosha katika somo hili. Mara kadhaa ningeingia kidogo kulifundisha, lakini kwa kweli sikufundisha hasa somo kamili.

Kwa hiyo, nyakati za karibuni, Bwana amenichochea nami naanza kufundisha zaidi katika eneo hili. Kitabu hiki ni sehemu ya kuchochewa huko na Bwana.

- Kenneth E. Hagin

Kwa mshangao wa wote, Marko alirudi nyuma na kutupa chini upanga wake. Watazamaji waligutuka na kushangaa. Waliduwaa hat...
11/08/2025

Kwa mshangao wa wote, Marko alirudi nyuma na kutupa chini upanga wake. Watazamaji waligutuka na kushangaa. Waliduwaa hata zaidi pale Marko alipomgeukia Mfalme na kunyoosha mikono yake.
"Mtawala Agusto," Alipaza sauti, "Mimi ni Mkristo. Nitapigana na Hayawani wa mwituni, lakini kamwe sitainua mkono wangu juu ya binadamu mwenzangu. Naweza kufa, lakini sitamwua mwanadamu mwenzangu."
Hapo kukaibuka manong’ono makubwa.
"Anasemaje?" Akauliza Marcelo. "Mkristo! Hiyo ilitokea lini?"
Nilisikia," akasema Luculo, "kwamba alipata kutembelewa na mmoja wa hawa Wakristo waliolaaniwa, na akajiunga na genge lao la uhaini. Wanatokana na jamii ya watu waliochacha. Ni dhahiri huenda kuwa ni Mkristo."
"Na Atakubali kufa kuliko kupigana?"
"Nd’o kawaida yao hawa walokole."
Hasira ilichukua nafasi ya mshangao katika nyuso za halaiki iliyokereketwa. Walijawa na ghadhabu kwamba mpiganaji mtumwa anathubutuje kuwasikitisha. Wahudumu wakakimbia kusimamia pigano lazima liendelee. K**a Marko hataki kupigana basi sharti aadhibiwe.
Lakini alikuwa thabiti pasipo silaha, akamsogelea Mwafrika, ambaye angeweza kumwua hata kwa mtupo tu wa ngumi yake. Uso wa mwafrika ukawa k**a wa ibilisi. Mshangao, furaha, na kishindo kilichomoza kwenye macho yake ya husuda. Akilishika barabara panga lake, akampiga Marko kwenye moyo.
"Bwana Yesu pokea roho yangu--" maneno haya yalitoka yakiwa yamelowa katika mkondo wa damu, na shahidi huyu wa Kristo, mpole lakini jasiri aliaga dunia na kujiunga na jeshi tukufu la wafia imani.

"Je! Kuna matukio mengi namna hii?" Aliuliza Marcelo.
"Mara kwa mara. Kila wanapokuwapo Wakristo. Watapigana na idadi yoyote ya wanyama. Wasichana wadogo watakuja kwa ushupavu kukutana na simba na chui, lakini hakuna hata mmoja ya hawa wendawazimu atakayepigana na binadamu. Watu wengi wamekasirishwa na Marko. Yeye ndiye bora ya wapiganaji wote, na kwa kuwa ni Mkristo ametenda k**a mpumbavu."
"Lazima itakuwa ni dini ya ajabu inayoweza kumfanya mpiganaji mtumwa kutenda namna hii," alisema Marcelo.
"Utakuwa na nafasi ya kujifunza kuhusu hilo."
"Kwa vipi?"
"Kwani hujasikia? Umechaguliwa kuwachimbua, baadhi ya hawa Wakristo wamejichimbia kwenye mapango, na ni lazima watafutwe na kuwindwa."
"Nafikiri wameshak**ata wa kutosha. Hamsini walichomwa moto asubuhi hii!"
"Na mia moja walikatwa vichwa juma lililopita. Lakini hiyo si kitu. Mji unafurikana na wao. Mfalme amedhamiria kuirejesha dini ya kale vikamilifu. Tangu waibuke hawa Wakristo ufalme umekuwa ukiporomoka, amefikia maamuzi kuwakomesha. Hawa ni laana, na sharti washughulikiwe ipasavyo, utafahamu hivi karibuni."
"Mimi sijawapo Rumi muda mrefu kuweza kufahamu," akasema Marcelo kwa upole," na sielewi Wakristo wanaamini nini hasa. Nimesikia karibu kila kosa na shutuma likitupwa kwao. Hata hivyo, ikiwa ni k**a usemavyo basi nitakuwa na nafasi ya kujifunza."
Lakini sasa tukio jingine lilinasa umakini wake.

"Ana mguso wa Midas" ndicho watu husema mara nyingi kuhusu mtu fulani aliyefanikiwa na mwenye neema. "Kila anachogusa hu...
11/08/2025

"Ana mguso wa Midas" ndicho watu husema mara nyingi kuhusu mtu fulani aliyefanikiwa na mwenye neema. "Kila anachogusa hugeuka kuwa dhahabu!"
Kulingana na hekaya za Kigiriki, Midas alikuwa mfalme aliyeishi Frigia Karne ya nane kabla ya Kristo. Alikuwa tajiri mno na alikuwa na dhahabu nyingi kuliko watu wote duniani. Alihifadhi sarafu za njano na chuma katika ghala kubwa chini ya kasri lake na alitumia masaa mengi kila siku kuihesabu na kuipanga hazina yake.
Lakini haijalishi ni kiasi gani cha dhahabu alichokusanya Midas na kuweka kwenye ghala lake, bado hakutosheka. Siku zote alitaka zaidi, na akatumia muda wake mwingi akiwaza jinsi ya kupata dhahabu nyingi zaidi.

Kulingana na hadithi, siku moja kiumbe mmoja akiwa amevaa mavazi meupe alimtokea Midas na kumtaka aombe anachotaka. Mara moja Mfalme akataka "mguso wa dhahabu" yaani kila anachogusa kigeuke dhahabu.
Asubuhi iliyofuata Midas alipoamka, aligundua mashuka yake ya kitani yalikuwa yamebadilika kuwa dhahabu safi! Alipumua kwa mshangao na kuruka toka kitandani. Halafu akagusa besela la kitanda, nalo likageuka kuwa dhahabu. "Ni kweli", akapiga kelele. "Nina mguso wa dhahabu!"
Akakimbia kuelekea ikulu huku akiparaza kuta na samani pande zote kwa mkono wake, zote zikageuka kuwa dhahabu kwa kuvigusa tu. Nje ya bustani, alipita kila kichaka na pori, akiyagusa maua makubwa kwa madogo, akitabasamu yalipogeuka kuwa dhahabu.

Huu ndio upande wa hadithi ambao watu wengi wanaukumbuka. Watu wengi wanaonekana kusisimka na wazo la kuweza kutengeza dhahabu ‐‐ utajiri usio kikomo ‐‐ kwa mguso tu wa kidole. Ni wazi, ndicho watu wanachofikiria wanaposema kuhusu "Mguso wa Midas".
Lakini hadithi ya Midas haikomei hapa ikimwacha kila mtu akiishi kwa furaha milele.

Hatimaye akiwa amechoka baada ya msisimko wa kugusa vitu mbalimbali na kuviona vikigeuka kuwa dhahabu, Midas aliketi chini kujisomea akiwa anasubiri staftahi. Lakini kitabu alichokishika mara moja kikageuka kuwa dhahabu. Halafu alipojaribu kula peasi, kijiko cha uji, na kipande cha mkate, vyote vikageuka na kuwa mapande magumu ya dhahabu! Hata maji katika kikombe chake yakageuka kuwa dhahabu.
Mfalme akash*tuka. "Sasa k**a hata chakula changu kinageuka dhahabu, nitawezaje kula tena?" Akapata wasiwasi. Muda si mrefu, bintiye Aurelia, akaingia chumbani. Alikuwa ndio kitu pekee alichokipenda k**a alivyopenda dhahabu zake. Aurelia akamkimbilia babaye, akipana mikono wazi na kumkumbatia, na kumbusu. Kwa mshangao na maumivu zaidi kwa Midas, binti yake aliganda kimya na kugeuka kutoka kuwa binti mcheshi, mwenye upendo hata kuwa nguzo ya dhahabu.
Mfalme alipiga ukelele wa maumivu, akiwa ameshikwa na bumbuazi ya yale yaliyokuwa yanatokea machoni pake. Alikuwa amepata alichokiomba, lakini ghafla akagundua alikuwa hataki tena kile alichokipata. Kwa bahati, huu sio mwisho wa hadithi ya Midas. Bado kuna upande wa mwingine wa hadithi.

Kiumbe yule aliyevaa nguo nyeupe alitokea tena ghafla na kuuliza, "Safi, Mfalme Midas, Je! Wewe sasa si mtu mwenye furaha kuliko wote?"
"Ooh hapana," aliomboleza Mfalme, "Mimi ndiye nuksi ya viumbe wote."
"Nini? Kwani sikukupa haja ya moyo wako ya mguso wa dhahabu?"
"Ndiyo, lakini ni laana tupu sasa," Midas alilia. "Yote ninayoyapenda kwa dhati yametoweka kwangu."
"Unamaanisha kusema kuwa ungependa kipande cha mkate au kikombe cha maji badala ya mguso wa dhahabu?" Akauliza kiumbe yule mwenye nguo nyeupe za kumeta-meta.
"Ooh, ndiyo!" Midas alilalama. "Nitatoa dhahabu zote duniani ikiwa tu binti yangu atarudishwa kwangu."
Kulingana na hadithi, kiumbe huyo alimwambia Midas akaoge kwenye chemchemi moja ya maji ambayo ingeosha mguso wake wa dhahabu. Pia alitakiwa kurudi na kiasi kidogo cha maji kumnyunyizia binti yake na vitu vingine alivyotamani virudi k**a mwanzo.

Basi mfalme mashuhuri Midas akaachilia mguso wake wa dhahabu na kufurahia katika urejesho wa vitu vya kawaida ya maisha --- familia, chakula, maji, uzuri wa asili. Midas alitambua kwamba vitu hivi ndivyo vyenye thamani kubwa kuliko dhahabu.

Charles G. Finney au Mwanauamsho Mkuu. Tangu zama za Mtume Paulo ni yeye tu ambaye asilimia 80 ya waongofu wake walidumu...
14/09/2023

Charles G. Finney au Mwanauamsho Mkuu. Tangu zama za Mtume Paulo ni yeye tu ambaye asilimia 80 ya waongofu wake walidumu katika wokovu. What a Man!!! Siku za leo naona watu wengi wanaokoka lakini hawadumu kanisani. Ni kwanini?
D.L. Moody alikuwa mtu mkuu wa Mungu lakini ni asilimia 50 tu ya waongofu wake walidumu katika wokovu. Sizungumzi kuhusu kudumu kanisani au dhehebu; nazungumza kudumu katika imani.
Siku za leo ni nani miongoni mwa mzunguko wa Wapentekoste ambaye watu wake wanadumu hata kwa asilimia 10?
Lakini Charles Finney si mchoyo, anatupa siri ya Uamsho mkuu aliofanya katika zama zake. Ikiwa ungependa kujua basi unahitaji kusoma siri hizo katika vitabu vyake...

"Mtu mmoja alimuuliza Mke wa Bill Graham k**a amewahi kuwaza kutalikiana na mumewe, akajibu 'Hapana; lakini nimewahi kuw...
06/09/2023

"Mtu mmoja alimuuliza Mke wa Bill Graham k**a amewahi kuwaza kutalikiana na mumewe, akajibu 'Hapana; lakini nimewahi kuwaza Kumuua"
Piga simu 0749 58 18 18 tukuletee kwa gharama zetu au fika mwenyewe dukani ujipakulie!!!

Address

Bora Street
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 08:00 - 18:00
Tuesday 08:00 - 18:00
Wednesday 08:00 - 18:00
Thursday 08:00 - 18:00
Friday 08:00 - 18:00
Saturday 08:00 - 18:00
Sunday 08:00 - 18:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Balm Bookshop posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category