16/03/2025
Kitu cha Kuzingatia Sana Kwenye Maisha Yako K**a Unahitaji Kupiga Hatua Mwaka Huu
Mwaka Jana, 2024, Najua Ulikuwa na Malengo, Si Ndio ?
Na Mwaka Huu Pia, 2025, Nafahamu Una Malengo Pia
Sasa, Nisikilize Kidogo...
Utafiti Uliofanywa na Chuo cha Harvad Unaonyesha Kwamba
- 83% ya Watu HAWANA Malengo
- 14% Wana Malengo LAKINI Hayajaandikwa
- 3% Tu Ndio Wenye Malengo Yaliyoandikwa
Na Unaweza Dhani Uko Kundi la 3%, Kumbe Hayo Uliyoyaandika HAYANA Sifa ya Kuitwa Malengo π
Au Ukadhani Uko Kundi la Asilimia 14, Kumbe Uliyonayo Kichwani Sio Malengo ni Wishes
[Kuna Tofauti Kubwa SANA Kati ya Malengo na Wishes.]
Sasa Leo, Siongelei Sifa za Malengo, Wala Tofauti ya Malengo na Wishes
Leo Acha Niongelee Kwa Ufupi Sana, *Umuhimu wa Kuandika Malengo Yako*
Nikuulize Hili Swali,
Huwa Ukienda Kwenye Semina/Mkutano/Kikao au Darasani na Daftari/Diary au Notebook
Je, Huwa Unaandika Kila Kitu Kinachosemwa na Mzungumzaji?
Jibu ni HAPANA
Bali, Huwa Unaandika Mambo Unayohisi ni Ya MSINGI Tu!
Sasa na Ubongo Wako Ndivyo Unavyozidi Kuuzoesha Kwamba Mambo ya Msingi Ndio YATAKAYOANDIKWA Katikati ya Mambo Mengi.
Tabia ya Ubongo Sasa Inakuwa ni Kukwepa Mambo Ambayo "Sio ya Msingi" na Kufanya "ya Msingi" Tu Ili Kutunza Energy.
Sasa, Turudi Kwenye Malengo Yako
K**a Haujayaandika, Unategemea Ubongo Wako Utakusaidia Kuyatimiza au Utakusaidia Kuyasahau?
Jibu Unalo
Kitu Kingine,
Malengo Yaliyoandikwa, ni Rahisi Sana Kuyafanyia Marejeo (Review) ili Kujua Umeyatimiza kwa Asilimia Ngapi
Pia, Kufahamu K**a Bado Uko Kwenye Malengo Yako au Umeshachepuka Mbali na Njia
Kitu cha Mwisho
Ukiwa Unaandika Malengo Yako, Hakikisha Unazingatia Vipaumbele
Lipi ni Lengo Muhimu Kuliko Yote, Lipi Linafuata kwa Umuhimu n.k
Ni Mapema Sana Kuyakatia Tamaa Malengo Yako, Bado Una Miezi Mingi Tu (Zaidi ya 8).
Stick to The Plan...
Ili Kujifunza Zaidi Kupitia Status Zangu Ninazopost Kila Siku, Karibu Unitajie Jina Lako Baada ya Kubonyeza Link Hapa Chini ππ½
https://wa.me/255627728867
au Nitumie Jina Lako Kwenda WhatsApp Namba 0627728867
Wako Katika Ujenzi Wa Fikra π§ π
Jeremiah Kisinza wa Kisinza Bookshelf and Summaries - KBS
Mafanikio ni Haki Yako π