14/08/2026
Unajua nini kuhusu dira ya 2050?
Unajua mtoto atakaezaliwa leo atakua na miaka 24?
Unajua tunaweza tukawa na idadi zaidi ya watu millions 120?
Unajua pato la taifa linatakiwa kuwa trillion 1 kwa mwaka? Leo ni billion 90 kwa mwaka.
Inabidi uchumi ukue kwa zaidi ya 11%.
Sector binafsi imebebeshwa jukumu hili kwa 70%
Vijana wanahitajka kuchangia kwenye safari hii kwa 70%
Tunahitaji sector ya kilimo ichangie Dira hii kwa zaidi ya 40% hii inawesekana kwa mwaka kilimo kikatupa zaidi ya billions 400. Nasema hivi kwasababu nchini ndogo k**a Uholanzi yenye ukubwa sawa na dodoma inaingiza billions 200 kwa mwaka mapato ya kilimo tu peke yake.
Tukiwa serious na kilimo pekee kinaweza kutufukisha kwenye lengo la pato la usd trilioni moja kwa mwaka hata kabla ya 2050.
Nataka kusema nini? Ni hivi pato la usd trilioni 1 kwa mwaka kwa nchi k**a Tanzania inawezakana ikiwa tutaamua kuwa serious na kuacha maneno na kufanya vitendo.
Lazima serikali ichukue hatua za makusudi kuhakikisha kundi kubwa la sector binafsi na vijana wanafanya kazi kwa kuwezeshwa kufanya kazi. Vijana wengi wana idea na uwezo wa kufanya kazi lakini wengi hawana mitaji na wanapishana na fursa k**a za kilimo. Nashangazwa na billions 200 za vijana alizotoa Rais mpaka sasa miezi 9 ziko bank zilitakiwa ziwe kazini zinazalisha. Punguzeni itafaki punguzeni vigezo lakini pia punguzeni matamasha wapeni vijana mitaji wafanyekazi nchi ianze hatua kuelekea 2050.