15/03/2025
HEBU TUIPE JINA HII COMBINATION
Hapa kuna volcano alafu kuna mkandaji alafu kuna mr MVP
niliwahi kusema na leo narudia tena hii combination hii kuna siku watu watalala na viatu na leo tumeonjeshwa ladha kidogo ila bado kabisa kuna siku timu itaondoka mapumziko haitorudi π€£
Hawa ni wachezaji watatu wenye tabia tofauti tofauti
KIBU ni mtaalamu wa kukokota mpira pia ana nguvu na ana uwezo wa kujikusanyia kijiji chake na akaondoka nacho pia kwa sasa kaboresha saba touch yake ya mwisho
AHOUA kwa sie tusie jua mpira ndo tunamchukulia poa ila jamaa ana usahihi wa matendo na slogan yake ni slow but sure na akifika ndani ya penalti box anakuwa ni hatari mnooo kuliko bomu la nyuklia pia huyu ni mtaalamu wa mipira iliyokufa
MPANZU huyu mwamba ni fullpackage ana kasi , ana nguvu ana vyenga anafunga ana asist pia ni mwepesi wa kufanya maamuzi
Huenda msimu huu tusiwafaidi sana kwakuwa mpanzu kaja dirisha dogo bado ajazoeana na wenzie pia ahoua bado ana ugeni wa ligi huku kibu nae aliikosa pre season sijui itakuaje msimu ujao wakienda pamoja pre season π€£π€£π€£