Christopher Mwashinga JR BOOKS

Christopher Mwashinga JR BOOKS TUNA-PROMOTE NA KUUZA VITABU VYA MCH. CHRISTOPHER MWASHINGA. Tangu mwaka 2009, maelfu ya vitabu vyak VITABU VYA MCH. CHRISTOPHER MWASHINGA
2. ELLEN G. WHITE
3.

TUNAUZA VITABU VYA AINA MBALIMBALI VIPYA NA VILIVYOTUMIKA:

1. BIBLIA ZA KILA AINA
4. VITABU VYA MAELEZO YA BIBLIA NA VINGINE VYA KIROHO
5. BIBLIOGRAFIA ZA WATU MAARUFU DUNIANI
6. VITABU VYA SHULE--KIDATO CHA KWANZA HADI CHA SITA
7. VITABU VYA AFYA NA VYA MAFUNZO YA MADAKTARI NA WAUGUZI
NA VINGINE VINGI

Congratulations kids from Bensian Daycare
10/12/2024

Congratulations kids from Bensian Daycare

06/12/2022

YALINDE MAWAZO YAKO
1.
Tazama yaliyo mema, chunga sana macho yako,
Sikiza yenye hekima, chunga masikio yako
Kwa umakini tazama, hiyo ndo milango yako,
Kilinda mawazo yako, utapata usalama.
2.
Kwa maombi na akili, yachunge mawazo yako,
Yaweza leta ajali, kuidhuru kesho yako,
Neno na yako kauli, yatoka moyoni mwako,
Kilinda mawazo yako, utapata usalama.
3.
Usiseme kwa kishindo, yachunge maneno yako,
Hubadilika matendo, yaachapo kinywa chako,
Yaweza leta uvundo, kuibua sokomoko,
Kilinda mawazo yako, utapata usalama.
4.
Hata uwe kidedea, yachunge matendo yako,
Hayo huwa mazoea, katika maisha yako,
Kila unapotembea, huitanda njia yako,
Kilinda mawazo yako, utapata usalama.
5.
Maswala ya kurudia, chunga mazoea yako,
Hujenga yako tabia, kubadili mwendo wako,
Kila unapokimbia, tabia i mbele yako,
Kilinda mawazo yako, utapata usalama.
6.
Kwa hali pia kwa mali, ichunge tabia yako,
Ni wako mstakabali, yaamua mwisho wako,
Nawe haichezi mbali, ni kitambulisho chako,
Kilinda mawazo yako, utapata usalama.
7.
Kwamba taishi mbinguni, pamoja na Mola wako,
Au taenda motoni, mwamuzi tabia yako,
Chunga usione soni, Mungu awe nguvu yako,
Kilinda mawazo yako, utapata usalama.
--------------------------------------------------
Christopher R. Mwashinga
(Sauti Toka Ughaibuni)

30/03/2022

The Seventh-day Adventist Church (SDA) has been working in Tanzania s… Selina Manumbu needs your support for The Comm. of African Adventist Writers & Readers

05/10/2019

Tumaini lenye baraka, ni kitabu kizuri mno , jipatie kopi yako ufurahie mashairi boraa zaidi ya kiroho.

Natumaini wote hamjambo. Napenda kuwajulisha Wapenzi wote wa vitabu vizuri vya mafundisho ya jinsi ya kukua kiroho na ku...
24/10/2018

Natumaini wote hamjambo. Napenda kuwajulisha Wapenzi wote wa vitabu vizuri vya mafundisho ya jinsi ya kukua kiroho na kumtumaini Bwana wetu Yesu Kristo kwamba, kitabu kipya kiitwacho KUMTUMAINI YESU kimeshatoka. Bwana apewe sifa kwa kuongoza mchakato mzima wa kuchapishwa kwa kazi hii ya muhimu ambayo watu wengi wamekuwa wakiisubiri kwa muda mrefu. Kwa sasa kitabu hiki kinapatikana hapa Marekani, wakati mipango ya kuhakikisha kinafika Afrika Mashariki mapema iwezekanavyo inapoendelea. Kwa wale wanaoweza kukipata mapema hapa Marekani, nawatakia usomaji mwema. Bei yake ni US $ 15.00 tu. Mbarikiwe sana.

28/08/2018

Wasomaji wangu wapendwa, natumaini hamjambo. Katika muda wa majuma machache yajayo, kile kitabu changu cha mahubiri kwa lugha ya Kiswahili kitatoka mitamboni. Kwa hiyo kaeni mkao wa kubarikiwa. Mungu awe nanyi daima.

31/01/2018

WANADAMU NI MUHIMU

Fedha dhahabu muhimu, katika hii dunia,
Japo kuwa ni adimu, ‘kipata vyasaidia,
Kuvisaka si haramu, kazi ukivifanyia,
Wanadamu ni muhimu, zaidi kuliko fedha.
*
Fedha k**a ukipata, Mungu akikujalia,
Jirani akikuita, shida akikulilia,
Usiujenge ukuta, wala kumpuuzia,
Wanadamu ni muhimu, zaidi kuliko fedha.
*
K**a ukipata shida, ugonjwa ukikujia,
Ni jambo la kawaida, msaada kulilia,
Kilio chako cha shida, fedha hazitasikia,
Wanadamu ni muhimu, zaidi kuliko fedha.
*
Lakini unapomwita, jirani atasikia,
Usiku wa saa sita, anaweza kukujia,
Bila ya kusitasita, dawa akakupatia,
Wanadamu ni muhimu, zaidi kuliko fedha.
*
Fedha zako na dhahabu, ulizojikusanyia,
Zaweza kosa adabu, pale unapozimia,
Na hiyo ndiyo sababu, ushauri zingatia,
Wanadamu ni muhimu, zaidi kuliko fedha.
*
Ukijifanya jeuri, fedha kutumainia,
Utaliona kaburi, bila ya kutazamia,
Utajiri ni mzuri, watu ukisaidia,
Wanadamu ni muhimu, zaidi kuliko fedha.
*
Hivyo jali wanadamu, heshima kuwapatia,
Wapatie na salamu, tena kwa kufurahia,
Ukiandaa karamu, waalike wote pia,
Wanadamu ni muhimu, zaidi kuliko fedha.
*
Kwani fedha si chochote, katika hii dunia,
Hazitendi mambo yote, unayoyatarajia,
Unavihitaji vyote, mapesa na watu pia,
Wanadamu ni muhimu, Zaidi kuliko fedha.
-----------------------------------
Sauti Toka Ughaibuni

24/01/2018

NJOO

Njoo Bwana wangu njoo, njoo nifute machozi,
Njoo asubuhi njoo, njoo ewe Mkombozi,
Njoo na mchana njoo, uwe wangu Kiongozi,
*
Njoo na jioni njoo, daima nakuhitaji,
Njoo mimi ni kondoo, wewe ndiwe Mchungaji,
Njoo wewe Komandoo, nifunze upambanaji.
*
Njoo nipatie nuru, mbele yangu kuna giza,
Njoo uniweke huru, dhambi zangu zaniliza,
Njoo komesha kufuru, dhoruba kuituliza.
*
Njoo nioneshe njia, wewe tangulia mbele,
Njoo nipe Bibilia, msalaba uwe mbele,
Njoo kunibarikia, daima nisonge mbele.
*
Njoo Bwana unilishe, mkate toka mbinguni,
Njoo ukanishibishe, niondokewe huzuni,
Njoo vazi univishe, nikatembee nuruni.
*
Njoo nishike mkono, k**a kitoto kichanga,
Njoo nilishe vinono, vitamu shinda karanga.
Njoo nione maono, maisha yajazwe mwanga.
*
Njoo twende kuhubiri, bado ninakungojea,
Njoo ninakusubiri, nifundishe kuongea,
Njoo wewe ni mahiri, saluti nakutolea.
*
Njoo kwa uwezo wako, unaotikisa mbingu,
Njoo utukufu wako, uangaze ulimwengu,
Njoo ili watu wako, wakulaki kwenye wingu.
*
Njoo imalize kazi, popote ulimwenguni,
Njoo kwa hiki kizazi, uikomeshe huzuni,
Njoo sinayo makazi, hapa si kwangu nyumbani.
*
Njoo univishe nguvu, kifo kamwe nisionje,
Njoo nishibe wokovu, nguvu za giza zivunje,
Njoo komesha uovu, usibaki hata punje.
*
Njoo Shetani akose, aambulie kokoto,
Njoo kisha umtose, katika ziwa la moto,
Njoo Bwana mtokose, abakie msokoto.
*
Njoo nikae winguni, nikapae kwa furaha,
Njoo dunia ni duni, mambo yake ni karaha,
Njoo nitwae mbinguni, nikapate kula raha.
*
Njoo unipe matunda, toka mti wa uzima,
Njoo Bwana ninapenda, maji yako ya uzima,
Njoo moyo unadunda, unatamani uzima.
*
Njoo Bwana nitembeze, barabara za dhahabu,
Njoo unibembeleze, nisikumbuke taabu,
Njoo unielekeze, niabudu kwa adabu.
*
Njoo Bwana niketishe, katika kiti cha enzi,
Njoo unitambulishe, kwa Mungu Baba Mwenyezi,
Njoo unisimamishe, nikuimbie utenzi.
---------------------------------------------
Sauti Toka Ughaibuni

Address

Benson
Dar Es Salaam
268

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Telephone

+255757699164

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Christopher Mwashinga JR BOOKS posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Christopher Mwashinga JR BOOKS:

Shortcuts

Share

Category