13/10/2023
IJUMAA, OKTOBA 13
YEYE ALIYE NA HEKIMA KULIKO SULEMANI
Bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu. 1 Wakorintho 1:24
🔰 Mtu huyu wa pekee ambaye Yohana Mbatizaji alikuwa amemtambulisha alikuwa ameishi nao kwa zaidi ya miaka thelathini, na hawakuwa wamemjua k**a ndiye Yeye aliyetumwa kutoka kwa Mungu. Huzuni iliwaingia wanafunzi kwa sababu walikuwa wameruhusu kutokuamini kulikokuwa kumeenea kuchachusha mawazo yao na kuweka ukungu katika ufahamu wao. Nuru ya giza la ulimwengu huu ilikuwa imedumu kung'aa katikati ya huzuni yake, na walikuwa wameshindwa kuelewa chanzo cha nuru hiyo kilikuwa wapi. Walijiuliza wenyewe kwa wenyewe k**a walikuwa wamechagua njia ambayo iliwafanya iwe muhimu kwa Kristo kuwakosoa. Walirudia mara nyingi mazungumzo Yake, na walisema, "Kwa nini tuliruhusu maslahi ya kidunia na upinzani wa makuhani na marabi kuchanganya fahamu zetu, kiasi kwamba hatukuweza kuelewa kuwa aliye mkuu zaidi kuliko Musa alikuwa miongoni mwetu, Yeye aliye na hekima zaidi kuliko Sulemani alikuwa akitufundisha? Masikio yetu yalikuwa mazito hatukusikia! Uelewa wetu ulikuwa dhaifu hatukuweza kuelewa!"
🔰 Tomaso hakuweza kuamini mpaka alipoingiza kidole chake katika vidonda vilivyosababishwa na mikuki ya maaskari wa Kirumi. Petro alikuwa alimkana katika kudharualiwa Kwake na kukataliwa. Kumbukumbu hizi za maumivu zilikuja katika mistari inayoonekana waziwazi. Walikuwa pamoja Naye, lakini hawakumwelewa wala kumkubali. Lakini mambo haya sasa yalitikisa mioyo yao walipogundua kutokuwa na imani kwao!
🔰 Makuhani na watawala waliungana pamoja na kujipanga dhidi yao, na waliwaleta mbele ya mabaraza na kuwatupa gerezani, wafuasi wa Kristo walifurahia "kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo" (Matendo 5:41). Walifurahia kuthibitisha, mbele ya wanadamu na malaika, kuwa walitambua utukufu wa Kristo, na walichagua kumfuata kwa gharama ya kupoteza vitu vyote.
🔘 Ndivyo ilivyo sasa k**a ilivyokuwa katika siku za mitume, kwamba pasipo mwangaza wa Roho wa Mungu, wanadamu hawawezi kutambua utukufu wa Kristo. Ukweli na kazi ya Mungu havithaminiwi na Ukristo unaopenda na unaolegeza masharti kuchukuliana na mazingira. Siyo katika njia ya wapenda raha, wapenda heshima ya kidunia au wanaofuata ulimwengu, ambamo utawakuta wafuasi wa Bwana. Wako mbele zaidi, katika njia za kazi ngumu, na kudharauliwa, na kuaibishwa, katika mstari wa mbele wa vita "juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho" (Waefeso 6:12).-The Desire of Ages, uk. 508.
Tafakari Zaidi: Nawezaje kuifanya hekima ya Yesu kuwa yangu, na kuiruhusu iongoze maisha yangu?
MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA
Tafadhali Subscribe, Like, Share & Comment
They often repeated His conversations, and said, “Why did we allow earthly considerations and the opposition of priests and rabbis to confuse our senses, so ...