Ndechi Inc

Ndechi Inc [email protected] Music website based in Tanzania. We post all new Hip-Hop/R&B tracks and videos. Follow us for daily updates.

Advertise/Inquiries To [email protected]

MJUE MJUSI (DINOSAUR) MKUBWA DUNIANI AMBAYE NI WETU(TANZANIA)Watu wengi hawajui kuhusu mjusi wetu, Leo tumfahamu vzuri. ...
21/10/2019

MJUE MJUSI (DINOSAUR) MKUBWA DUNIANI AMBAYE NI WETU(TANZANIA)

Watu wengi hawajui kuhusu mjusi wetu, Leo tumfahamu vzuri.
Kipindi cha ukoloni, Tanzania ilishawahi kuwa koloni la mjerumani, na katika kipindi hicho ndo mabaki ya mifupa ya mjusi wetu yaligunduliwa na wajerumani.

Mjusi wetu aligunduliwa mwaka 1907-1913 katika vilima vya Tendaguru mkoani Lindi na mgunduzi mjerumani aitwaye WERNER JANENSCH ambaye alikuwa mtaalamu wa mabaki ya wanyama.

Mjusi wetu alikuwa na mifupa zaidi ya 5000, yenye uzito wa tani 250 na hii imepelekea kutambulika na GUINNESS k**a mjusi mkubwa zaidi duniani kutokana na kuwa na urefu wa mita 13.27 (GUINNESS WORLD RECORDS). Baadaye uongozi wa kijerumani nchini uliamua kusafirisha ile mifupa kwende Berlin ujerumani mwaka 1909-1913 na kuhifadhiwa katika NATURKUNDEMUSEUM na imekuwa kivutuo kikubwa x**a kwa watalii na inawaingizia sana kipato ujerumani k**a chanzo chao cha utalii na hakuna hata shilllingi moja Tanzania tunapata ingawa ni Mali yetu(shamba la bibi)....!!!! *MSIMAMO WA SERIKALI* (Majadiliano bungeni bajeti 2016/2017)

mwaka 2016 wabunge walitaka mjusi huyu arudishwe. Majibu ya serikali yalikua k**a ifuatavyo; (1) Serikali ya Tanzania haina uwezo wa kiteknolojia kumtunza na makumbusho yetu hayana uwezo na vifaa vya kumtunza. (2) Njia nzuri ni kuongea na serikali ya Ujerumani kuona Tanzania itanufaikaje. (3) Serikali ya Ujerumani imekubali kuwasomesha watanzania watatu.

BARUA ALIYOANDIKA BILIONEA WA APPLE, STEVE JOBS KABLA YA KUFARIKI “Nilifikia kilele cha mafanikio katika biashara dunian...
18/10/2019

BARUA ALIYOANDIKA BILIONEA WA APPLE, STEVE JOBS KABLA YA KUFARIKI “Nilifikia kilele cha mafanikio katika biashara duniani. Katika macho ya watu wengine, maisha yangu ni kielelezo cha mafanikio. Hata hivyo, mbali na kufanya kazi, nina furaha ndogo. Kwa jumla, utajiri ni uhalisia tu wa maisha ambayo nimeyazoea.
Wakati huu ambao nimelala kitandani nikiwa mgonjwa na kuyakumbuka maisha yangu yote, ninagundua kwamba ufahamu utajiri nilionao umefifia kwa kuwa hauna maana wakati kifo kinakaribia.
Nikiwa gizani, ninautazama mwanga wa kijani kutoka katika mashine zinazonisaidia kuendelea kuishi na kusikia sauti za muungurumo wake, ninasikia na kuhisia pumzi za Mungu na za kifo zikinikaribia…
Sasa nafahamu kwamba tunapolimbikiza utajiri wa kutosha maishani mwetu, inatupasa kufuatilia mambo mengine ambayo hayahusiani na utajiri…
Kiwe ni kitu fulani ambacho ni muhimu zaidi:
Labda ni uhusiano, labda ni sanaa, labda ni ndoto inayoanzia katika siku za ujana…
Kutafuta utajiri muda wote utamwingiza mtu katika maisha yasiyofahamika, k**a mimi.
Mungu alitupa hisia za kutambua pendo katika kila moyo wa mtu, si mauzauza yanayoletwa na utajiri.
Utajiri nilioupata maishani mwangu siwezi kuondoka nao.
Ninachoweza kuondoka nacho ni kumbukumbu zilizojaa upendo.
Huo ndiyo utajiri wa kweli utakaokufuata, utakaoungana nawe, ukakupata nguvu na mwanga wa kusonga mbele.
Upendo unaweza kusafiri maelfu ya maili. Maisha hayana kikomo. Nenda unapotaka. Fika katika kilele unachotaka kufika. Yote yamo moyoni na mikononi mwako.
Ni kitanda gani chenye gharama zaidi duniani? Ni kitanda wanacholalia wagonjwa…
Unaweza kumwajiri mtu akaendesha gari lako, mtu akakuingizia fedha lakini huwezi kumpata mtu wa kubeba ugonjwa wako.
Vitu vilivyopotea vinaweza kupatikana. Lakini kuna kitu kimoja ambacho hakipatikani pindi kikipotea ni Maisha.

Mtu anapokwenda katika chumba cha upasuaji, atagundua kwamba kuna kitabu kimoja ambacho bado hajamaliza kukisoma “Kitabu cha Maisha ya Afya”.
Hata tukiwa katika daraja gani la maisha hivi sasa, muda ukifika, tutakabiliana na siku ambapo pazia la maisha litashuka.

Thamini Upendo kwa familia yako, mpende mwenza wako, marafiki zako. Jitambue vyema. MWISHO WA BARUA.!!

(SEHEMU YA KWANZA)HILI BOMU NDIO MFALME WA MABOMU YOTE KUWAHI KULIPULIWA ULIMWENGUNI, NDILO BOMU HATARI ZAIDI DUNIANI.Tu...
17/10/2019

(SEHEMU YA KWANZA)

HILI BOMU NDIO MFALME WA MABOMU YOTE KUWAHI KULIPULIWA ULIMWENGUNI, NDILO BOMU HATARI ZAIDI DUNIANI.

Tumekuwa tukisikia mabomu mabomu tokea tunaanza kujitambua hadi sasa , ila ni kwa mara chache tumepata kujiuliza uzito na uhatari wa mabomu hayo. Katika makala hii ninakuletea kiufupi bomu hatari zaidi kuwahi kutengenezwa na mikono ya mwana wa Adamu.
Mwanzoni mwa miaka ya 50 na 60 dunia ilishuhudia mpasuko mkubwa baina ya Mashariki na Magharibi, kipindi hiki ndio kilikuwa cha kupona vidonda baada ya kutoka kujeruhiwa na Vita kuu ya pili ya dunia, vita ambayo mtata Adolf Hi**er aliihenyesha dunia, vita ambayo kwangu mbabe huyu wa Kijerumani ninampa "credit" kwa kuionyesha dunia umahiri wake na commitment yake aliyokuwa ameiweka ili kuifanya Ujerumani kuwa super power duniani. Baada ya Ujerumani kuangushwa katika vita hii mataifa ya Marekani na Urusi kwa upande mwingine yaliwagombania wataalamu na Wanasayansi wa Ujerumani na kuwamishia katika nchi zao ili wakahamishie utaalamu wao katika nchi zao. Oparesheni hii ilipewa jina maarufu la "PAPERCLIP". Katika oparesheni hii Marekani iliwakusanya wataalamu, wahandisi na wanasayansi zaidi ya 1600 wa Kijerumani na Urusi pia iliwachukua wengi k**a mwenzake marekani.
Katika Mkutano mkuu wa umoja wa mataifa (United Nations General Assemby) wa mwaka 1960, Rais wa Urusi kipindi hicho bwana NIKITA KHRUSHCHEV aliikemea Marekani kwa maneno makali na kuahidi kuwaonyesha kuwa Urusi ni nani. Baada ya ahadi hiyo Bomu zito la TSAR BOMBA lilianza kuzaliwa katika mawazo ya wanafizikia wa Kirusi waliokuwa kwa wingi wamechukuliwa kutoka Ujerumani baada ya kuanguka kwa utawala wa Hi**er pamoja na wanasayansi wenyeji wa Urusi walianza kazi maabara ya kuzalisha kitu cha aina yake duniani.
Bomu hili liliandaliwa kuwa likilipuka litoe mlipuko wa uzito wa Megatoni (Tani Millioni) 100 lakini baada ya kukamilika liliweza kulipuka katika na kutoa mlipuko wa uzito kiasi cha Tani millioni 50, watalaamu wanasema k**a lingeweza kuachiwa kulipuka kwa intensity ya tani milioni 100 basi lingeweza kuipasua dunia katika vipande viwili mithili ya yai na hivyo kuiathiri hata Urusi yenyewe.
INAENDELEA..!!!
Like page yetu kwa kubonyeza kitufe cha like ili upate sehemu inayofuata.

26/08/2019

Waraka wa James Obedi

Afrika kwa sasa inashuhudia aina mpya ya utumwa kupitia Ukristo ikitwa *ulokole*.
Aina hii ya utumwa wa imani imewafanya watu wengi kuwa wavivu wa kufikiri na uwezo wa kutafakari mambo umedumazwa.

Baadhi ya wachungaji wa kilokole wamejipa uungu mtu. Wanapenda kutukuzwa, kuabudiwa na kusujudiwa. Wanajitukuza wao zaidi kuliko kumtukuza yule wanayemhubiri.....Yesu Kristo.

Wachungaji wa aina hii hawawezi kuongelea mafanikio ya watu weusi k**a Barack Obama, Serena Williams, na Usain Bolt. Hawawezi kuongelea wagunduzi waliosaidia ku-transform dunia k**a kina Albert Einstein, Steve Jobs na wengine. Hawawezi kuongelea Wanasayansi walio-dedicate maisha yao na wengine kufia maabara wakitafuta dawa za kutibu magonjwa mbalimbali yanayoisumbua Afrika.

Hawawezi kuongea kuhusu wanafasihi vijana k**a Chimamanda Ngozi na Ben Okri, au wanafasihi wakongwe k**a Chinua Achebe na Ngugi wa Thiong'o.

Kila pembe ya dunia kuna watu waliofanikiwa kutokana na maarifa, bidii, ubunifu, na weledi. Wapo wafanyabiashara, wanasiasa, wanafasihi na hata wanasayansi wanaofanya mambo makubwa ya kuisaidia dunia yetu. Lakini wachungaji wa Afrika hawatawaongelea watu wa aina hii.

Wao wataongelea mtu aliyepata kazi kimiujiza licha ya kukosa sifa za kupata kazi hiyo, kwa sababu tu aliombewa na kupewa mafuta ya upako siku ya interview ya kazi.

Wataongelea kuhusu kijana aliyetoa mshahara wake wote kwa miezi mitatu mfululizo kwa Mchungaji wake k**a mbegu ya mafanikio, baadae akawa 'Boss' kazini.

Au wataongelea kuhusu kijana aliyefeli sekondari lakini baada ya baba yake kumalizia ukarabati wa nyumba ya Mchungaji, alipokea barua ya kupata 'admission' chuo kikuu bila hata kurudia mitihani.

Wachungaji hawa hutumia 'miujiza na shuhuda feki' k**a njia ya kuwafumba akili wafuasi wao. Kule Afika kusini kuna Mchungaji alidanganya kufufua mtu. Hata alipoomba msamaha baadae, bado kuna waumini wanaendelea kumuamini na kumsujudu.

Na wamegundua haya ndio mahubiri yanayopendwa sana huku Afrika. Hawataki kuhubiri kuhusu Aliko Dangote alivyoanza biashara na magumu aliyopitia mpaka mafanikio aliyopo sasa.

Wanahubiri kuhusu mama Janeth aliyekua mama Ntilie huko Enugu, lakini alipotumia mtaji wake wote wa shilingi laki 5 kununua mafuta ya upako kutoka kwa nabii fulani, ghafla biashara yake ikakua na sasa anamiliki mahoteli makubwa pande zote za nchi. Yaani bila mtaji, bila business plan, bila timeline ghafla tu akamiliki mahoteli. Na waumini watashangilia kwa sauti na kuitikia kwa kusema ameeeen.

Aina hii ya ukristo imepanda mbegu ya uvivu wa kufikiri kwa vijana wengi wa Afrika ambao wanalazimishwa kumuona Mungu k**a Mfadhili wa wavivu, au wasiostahili. Kwamba mwanafunzi hata asiposoma anajua akipewa mafuta ya upako atafaulu tu siku ya mtihani. Mfanyabiashara hata asipokua mbunifu anajua akienda kwa 'baba wa miujiza' biashara yake itapanuka ghafla bin vuu. Mfanyakazi hata asipowajibika kazini anajua akitoa fungu la kumi kwa 'Dokta Upako' atapanda cheo.

Kwa baadhi ya makanisa Afrika namna pekee ya kufanikiwa ni kufanya kile wanachokiita kupanda mbegu, kupaka mafuta ya upako au kunyunyuziwa maji ya baraka. Eti wanaofanikiwa haraka ni watu 30 wa mwazo wanaokimbilia mbele ya kanisa kila mmoja akiwa ameshika noti ya dola 100.

Aina hii ya mahubiri inawafanya watu waamini kwamba Mungu hawapendi wanaojituma na kuwa wabunifu katika kazi, badala yake anawapenda zaidi wanaotoa zaka, sadaka, malimbuko na fungu la 10 hata k**a ni wavivu. Hii sio sawa hata kidogo kwa sababu Biblia inakataa uvivu kwa nguvu zote (Mithali 12:27)
_
Watu wanaaminishwa kwamba ukishatoa sadaka kanisani unaweza kuamka kila siku asubuhi ukapayuka 'Mimi ni Milionea' halafu ukavuta shuka na kuendelea kulala fofofo, ukisubiri sadaka uliyotoa ikupe muujiza wa kuokota hela, ili upate mtaji wa biashara unayoiwaza.

Mtu huna kazi, huna biashara wala wazo la biashara, huna ujuzi, huna elimu, lakini kila siku unashinda kanisani kumsikiliza Mchungaji anayesema kesho utakua milionea na wewe unasema "Baba napokea/Dady I receive". Huu ni utani.

Waambieni wanaofanya huu utani kwa kofia za Uchungaji, Uaskofu, Unabii au Utume kwamba wanamkosea Mungu. Waambieni Mungu wetu ni Mungu wa kanuni, na hana kanuni ya kuwabariki wavivu. Tuache kufundisha waumini wetu kwamba uvivu unalipa kupitia miujiza.

Mafanikio ni matokeo ya bidii, ubunifu na weledi. Biblia inazungumzia kuhusu karama. Hebu kila mtu atumie karama alizopewa kwa bidii, ubunifu na weledi aone k**a hatafanikiwa. Sio sahihi kuwaambia watu wabweteke tu na kusubiria mafanikio k**a kusubiria daladala kituoni kwa sababu tu wamepakwa mafuta ya upako.

Mungu alishatubariki tangu wakati wa uumbaji wetu. Ni wajibu wetu kujibidisha katika yale tufanyayo ili baraka zake ziambatane nasi (Kumb 28:6).

Wazungu na Wachina wanazidi kushindana katika kuitawala dunia kwenye mambo mbalimbali kuanzia viwanda, biashara, sayansi na teknolojia. Sisi tuko 'busy' kununua maji ya upako tukiamini yatatufanya tuwe k**a Jack Ma au Bill Gates. Upuuzi.

Tumeumbwa kuitawala hii dunia (Mwanzo 1:28). Tutumie vipawa na karama tulizopewa ili kutimiza kusudi hilo la Mungu. Tusiruhusu Askofu, Mchungaji, Nabii, mtume au kiongozi mwingine yeyote wa dini atutawale akili zetu kwa kutuhubiria mafanikio ya miujiza. Wao wanashi kifahari kwa sadaka za waumini wao, huku waumini hao wakiendelea kuwa mafukara wa kutupwa.

Biblia inasema kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa (Mithali 1:7). Tutafute maarifa, tufanye kazi kwa bidii, na tumuabudu Mungu katika riho na kweli. Kwa kufanya hivyo tutapata MAFANIKIO katika mambo yote tuyafanyayo. Mungu akubariki unayesoma ujumbe huu.

by
James Obedi

Beijing Daxing International Airport inaanza kutumika Sept 30. Itakuwa moja ya airport kubwa Duniani, yenye uwezo wa kup...
15/08/2019

Beijing Daxing International Airport inaanza kutumika Sept 30. Itakuwa moja ya airport kubwa Duniani, yenye uwezo wa kupokea wasafiri 72m kwa mwaka na mizigo ya kufikia tani milioni 4. Itakuwa na runway 4 na terminal ukubwa wa viwanja 97 vya mpira!! ————————————————————————————ikianza kutumika hii, Jiji la Beijing, China litakuwa na viwanja viwili vikubwa. Yani jiji moja lenye ‘two world largest international airports’! Airport iliopo sasa imezidiwa inapokea wasafiri karibia 100m kwa mwaka!
———————————————————————————

Warusi ndio walikuwa wakwanza kurusha vyombo Mars mwaka 1971. Hata hivyo vilifia huko——————————————————————————Uingereza...
11/08/2019

Warusi ndio walikuwa wakwanza kurusha vyombo Mars mwaka 1971. Hata hivyo vilifia huko
——————————————————————————Uingereza ilirusha chombo mwaka 2003 kikafia huko pia
——————————————————————————Marekani wamesharusha vyombo vinne kwenda Mars mpaka sasa. Vitatu vimeshafia huko kimebaki kimoja tu wanachokiita ‘’Curiosity”. Bahati nzuri vyote vilifanikiwa kutuma picha Duniani kabla ya kufa. Sasa wanajiandaa kurusha vyombo viwili zaidi ‘’ExoMars’’ na ‘’Mars 2020’’
——————————————————————————-Vyombo hivi ni gharama! chombo kimoja kinagharimu takribani Trilioni TSh 5.9 ($2.5B)
———————————————————————————
Kuna siku tutakutana na wenzetu? !! Niachie mtazamo wako kwenye comment section.
————————————-

Tarehe k**a ya leo miaka 50 iliyopita binadamu watatu;  Neil Armstrong, Buzz Aldrin na Michael Collins kutoka Marekani w...
11/08/2019

Tarehe k**a ya leo miaka 50 iliyopita binadamu watatu; Neil Armstrong, Buzz Aldrin na Michael Collins kutoka Marekani waliondoka Duniani kuelekea mwezini wakiwa hawana uhakika k**a watafanikiwa kurudi!
————————————————————————— Walitumia chombo kilichoitwa Apollo 11. Siku nne baadae, (tarehe 20) walifika mwezini na wawili kati yao; Armstrong and Aldrin wakawa binadamu wakwanza kukanyaga ardhi ya mwezini. Collins hakushuka nje ya chombo. Wote walifanikiwa kurudi Duniani ———————————————————————————Hivi na sie tutafikia hatua hiyo lini?
———————————————————————————
For technology update like ukurasa wetu hapo juu kwa kubonyeza kitufe cha like page.

Address

Chekereni Alongside Munio Headquarters
Dar Es Salam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 22:00
Thursday 09:00 - 22:00
Friday 09:00 - 22:00
Saturday 09:00 - 22:00

Telephone

0659520960

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ndechi Inc posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Ndechi Inc:

Shortcuts

Share