11/02/2023
KIDATO CHA TANO 2023
DCT MVUMI SEC SCHOOL
DODOMA-TANZANIA.
Combination/ Tahasusi!
PCM, PCB, CBG, EGM
HGL, HKL, HGK, HGE na ECA
NANI ANAWEZA KUPATA NAFASI ZA KIDATO CHA TANO DCT MVUMI SEC SCHOOL?
Mwanafunzi YEYOTE (Mvulana au Msichana) aliemaliza kidato cha nne na kufaulu kwa kiwango cha...
Division 1√
Division 2√
Dision 3 √
SIFA GANI MAHUSUSI ANATAKIWA KUWA NAZO MUOMBAJI??
1. Muombaji awe na ufaulu usiopungua alama CCD kwenye Masomo Matatu yanayounda Combination anayotaka kusoma.
DCT MVUMI INAMILIKIWA NA NANI??
DCT Mvumi secondary school yenye usajili S.0804 inamilikiwa na Kanisa Anglicana Tanzania Dayosisi ya kati (DCT). Ni shule Kongwe na yenye mafanikio Makubwa kwani nimmiongoni mwa shule Kumi bora kimkoa, ni ya Mchanganyiko yaani wavulana na wasichana, Kutwa na Bweni na inapokea wanafunzi wa dini zote.
SHULE IKO WAPI??
DCT MVUMI SECONDARY SCHOOL ipo Mkoani Dodoma Wilaya ya CHAMWINO, Katika kijijini Maarufu cha Mvumi Mission nyumbani kwa Waziri mkuu wa zamani ndugu John Samwel Malecela, ni KILOMETA 33 tu KUTOKEA JIJINI DODOMA. Mwendo wa dakika 40 kwa Usafiri wa Umma na dakika 30 TU kwa usafiri binafsi.
UNAFIKAJE DCT MVUMI SEC SCHOOL??
Ukiwa jijini Dodoma unaenda Soko kuu la Majengo, hapo utauliza stendi ya daladala za kwenda Mvumi, Gari zipo muda wote kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa tatu usiku. Na kwa usafiri binafsi Ulizia njia ya kwenda Hospitali ya DCMC -Ntyuka, hiyo ndio njia ya kwenda mvumi mission!
KWANINI MWANAO AJIUNGE NA DCT MVUMI SEC SCHOOL?
DCT Mvumi secondary inao Walimu mahiri, mazingira tulivu na bora ya kujifunzia, Maabara za kutosha za masomo ya sayansi, sanaa na computer. Maktaba nzuri yenye vitabu vyote Muhimu, huduma za afya za uhakika kwani imepakana na Hospitali kubwa ya Mvumi inayomilikiwa na Kanisa Anglican Pia, Ina Viwanja vya michezo yote, Huduma za umeme na maji za uhakika Muda wote kwani shule ina kisima chake na jenereta la dharula endapo umeme wa Tanesco utakatika. Shule ina Utaratibu mzuri wa kuruhusu wanafunzi wa dini na madhehebu yote kuabudu, Malezi Bora kwetu ni Kipaumbele.
ADA VIPI??
Ada zetu ni rafiki sana! Za kitanzania, zinalipika na zinazungumzika!
KARIBU SANA.
NAFASI KWA VIDATO VINGINE ZINAPATIKANA??
DCT MVUMI SEC SCHOOL inazo nafasi chache za kuhamia kwa kidato cha PILI (watafanya interview), cha TATU ( wenye Division 1 au 2 kwenye mtihani wa Taifa wa kidato cha Pili) na kidato cha TANO kwa Tahasusi za PCB, PCM, CBG, EGM ,HGE, HGL, HKL , HGK na ECA (Matokeo yao ya NECTA yatatumika).
FOMU ZA KUJIUNGA ZINAPATIKANA WAPI KWA GHARAMA GANI?
Fomu za kujiunga na shule zinapatikana sehemu zifuatazo;
1. SHULENI Dct Mvumi -Mvumi mission, Dodoma
2.Mackay House, Chumba namba 23 Jijini Dodoma.
3.Unaweza kupakua fomu popote ulipo kupitia Tovuti ya shule ambayo ni www.dctmvumi.sc.tz
GHARAMA YA FOMU JE??
Utachangia SH 10,000 TU.
Tupigie Muda wa Kazi tukupe Maelezo zaidi...
0717243199 0714278470 0714772095
DCT MVUMI SEC SCHOOL, EDUCATION IS LIBERATION