29/07/2016
Juzi kuna jamaa yangu kupitia akaunti yake ya fesibuku akatangaza kuwa analiuza gari lake.
Basi akapigiwa simu nyingi sana na watu kibao wakitaka kununua gari hilo.
Akanipigia simu usiku na kuniambia kuwa kesho yake tuonane asubuhi na mapema yaani jana kwani kampata dada mmoja anataka kulinunua gari hilo hivyo nimsindikize akamwonyeshe na niwe shahidi wauziane.
Nikamtania sasa ndugu k**a shahidi utanipa asilimia ngapi?
Akaniambia usijali fuledi wewe twende gari likitoka una laki tatu zako hapa za haraka si wajua tena mjini mpipango na wenye kuiweka mipango ni sisi?
Basi jana mida ya saa nne akanifuata nyumbani na tukaondoka kwenda kuuza gari wakati huo mie nimewaambia nyumbani waandae maji ya kunyonyolea kuku kwani nilijua haitachukua hata saa gari litakuwa nimeuzika kwani ni jipya na mie nilijua nitapokea ka hela kangu ka ushahidi plus hamu ya kuku safari ikaanza.
Tukaondoka na tukiwa njiani yule dada akawa ameshatupigia simu zaidi ya mara nne vile mpaka mie nikaanza kumlaumu rafiki yangu kwa kuchelewa ili tumwahi mteja.
Akatuelekeza alipo na hatimaye tukafika bar moja na kukutana na dada mmoja aliyeonekana ni mishentown sana.
Kumwonyesha gari akasema hili ni bonge la gari na wakalitesti na jamaa yangu wakati huo kashatuagazia bia moja moja na supu.
Baada ya kulikagua na kuridhika akamwambia jamaa kuna mteja amabye ni mme wa yule dada anakuja pale na yeye huwa malipo anafanya moja kwa moja kwa nia ya mtandao hivyo yeye anahitaji laki tano tu ya kumleta mteja hivyo rafiki ajue k**a ataiseti kwenye bei au lah.
Saa moja baadae akaja jamaa mmoja ambaye alidaiwa kuwa mteja wakaliangalia gari naye akaridhika sana na wakaanza kuulizia kadi ya gari tukamwonesha akaridhika na kutupa round za bia pale tukisuribi sasa wafanye mambo tusepe.
Baada ya kula pale jamaa akatoa wazo waondoke na rafiki mwenye gari wakalipe bank na wakija iwe ni kuandikishana tu.
Mie nikatoa wazo ni vyema tumwite na mwite au twende kwa wakili, jamaa akadai poa poa ni wazo zuri na akaomba mie na mkewe tubaki tuendelee kunywa bia na kuagiza tutakacho.
Wakiwa wanataka kutoka yule mama akamwita rafiki yangu mwenye gari na kumwambia kwa kuwa wewe unaenda kulipwa huko basi nipe changu hapa hapa.
Jamaa akajikaguaa wee akawa na laki mbili na nusu cash ambayo alitakiwa kumlipa mdeni wake mmoja, mimi nikamwambia jamaa unajua nilitoka haraka home hivyo sina wala kwenye simu na hata hivyo simu yenye miamala iko home.
Basi mama akasema, "plz nakuamini ukiniletea uhuni utahama mjini"
Kisha akamwambia nitumie ya juu kwenye laini yangu ya simu na jamaa wakaondoka mie na mama tukabaki pale tukila bia na mie naletewa naweka kinywani tu.
Robo saa baadae yule dada aka............................... endelea kwa kufuata link http://tabasamunafuledi.blogspot.com/2014/07/soma-jinsi-jamaa-alivyolizwa-na-wajanja.html