31/10/2021
Kabichi ni moja ya mazao
yaliyomo katika jamii ya
mimea inayojumuismimea inayojumuisha
mimea ya cauliflower
kabichi Kwa kawaida
kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa
ajili ya kutoa mbegu
hukuzwa zaidi ya msimu
mmoja. Endapo inalimwa
sehemu yenye maji ya
kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka. Kichwa cha kabichi
kinapofunga vizuri,
hutumika k**a chakula
na huvunwa baada ya
kufunga na kukomaa
vizuri. Kabichi ni zao linalopendelea hali ya
ubaridi. Zao hili hustawi
na kutoa mazao mengi na
bora kwenye sehemu
zenye miinuko ya kuanzia
mita 1200 hadi 1900 kutoka usawa wa bahari. Nchini Tanzania kabichi
hustawishwa zaidi katika
mikoa ya Kilimanjaro,
Arusha, Morogoro, Tanga,
Iringa na Mbeya. Kabichi
ina madini aina ya chokaa, kambakamba,
protini na maji kwa wingi.
Mboga hii inaweza kuliwa
bila kupikwa au
kuchemshwa kwa
kutengeneza kachumbari. Pia inaweza kupikwa
pamoja na vyakula k**a
vile nyama na maharagwe HALI YA HEWA
INAYOFAA KWA KILIMO
CHA KABECHI Kwa kawaida kabichi
huhitaji hali ya hewa
iliyotulia na kavu ili
kuweza kufanya vizuri.
Lakini kabichi humudu
mazingira mengi. Mazingira yenye baridi
kali au joto kali huharibu
ukuaji pamoja na uzaaji
wa kabichi. Udongo
wowote wenye virutubisho
hai unafaa kupandia kabichi kinachotakiwhai unafaa kupandia kabichi kinachotakiwa ni
kuhakikisha kuwa udongo
unaweza kuupa mmea
chakula kiasi
kinachohitajika kukua na
kuzaa. Matumizi ya maji yanatakiwa yaangiliwe
vizuri ili kuhakikisha kuwa
maji hayazidi wala
kupungua kwani maji
mengi husababisha mizizi
kuoza, ni chanzo cha magonjwa na mmea
kudumaa.