Baraka Makali

Baraka Makali Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Baraka Makali, Shopping & retail, Sumbawanga.

13/07/2023

With ma love family 💕

03/01/2023
UGONJWA WA KISONONO(GONORRHEA)Ugonjwa wa Kisonono (Gonorrhoea) ni ugonjwa unaoshambulia watu wengi, wanaume kwa wanawake...
30/07/2020

UGONJWA WA KISONONO(GONORRHEA)

Ugonjwa wa Kisonono (Gonorrhoea) ni ugonjwa unaoshambulia watu wengi, wanaume kwa wanawake. Ni ugonjwa unaotibika ingawa kwa miaka ya karibuni, wadudu wa ugonjwa huu wameonyesha kuanza kutosikia tiba zinazotolewa.

Chanzo Cha Kisonono (Gonorrhoea)

Kisonono ni ugonjwa unaoambukiza kwa ngono – sexually transmitted infection (STI) – na unasababishwa na bakteria
aitwaye Neisseria gonorrhoeae au gonococcus.
Bakteria huyu hupenda kuzaliana kwenye maeneo ya joto, yenye unyevunyevu yakiwemo maeneo ya shingo ya uzazi (cervix),
nyumba ya uzazi (uterus),
mirija ya uzazi (fallopian tubes) na mrija wa kutolea mkojo nje (urethra).

-Bakteria hawa pia huweza kuzaliana kwenye
mdomo,
mkundu na
mara chache kwenye koo na macho.

-Kimsingi bakteria hawa hupatikana kwa wingi katika shahawa na usaha unaotoka katika uume wa mwanamme mgonjwa na

katika majimaji ya ukeni.

Bakteria hawa huambukiza kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa njia zifuatazo: Ngono zembe kupitia uke, mdomo au mkundu.
Kuchangia vifaa vya kujistarehesha ambavyo havikuoshwa au kufunikwa na kondomu, k**a vi*****rs na vimwanasesere
vya aina nyingine.

Mama mjamzito mwenye maambukizi anaweza
kumwambukiza mtoto anayezaliwa na endapo mtoto huyo hatapewa tiba, anaweza
kupata upofu wa kudumu.

Hivyo, mama mjamzito mwenye maambukizi anatakiwa apewe tiba kabla ya kujifungua.

Dalili za gono kwa mwanaume

Kutokwa na uchafu uumeni wenye rangi nyeupe, njano au kijani unaofanana na usaha
Maumivu kwenye mapumbu
Maumivu wakati wa haja ndogo
Kutokwa na uchafu kwenye
mkundu, kuwashwa, kutokwa damu wakati wa haja kubwa
Koo kukauka, kuwashwa, kumeza kwa shida au uvimbe shingoni
Maumivu kwenye macho, macho kutopenda mwanga mwingi na kutokwa uchafu machoni unafanana na usaha Maumivu na kuvimba kwenye sehemu za maungio ya mifupa

Dalili Za Kisonono Kwa Mwanamke
Maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa. Homa Kutokwa uchafu ukeni wenye rangi ya njano au kijani Kuvimba eneo la uke Kutokwa damu katikati ya siku za mwezi Kutokwa damu baada ya kufanya tendo la ndoa Kutapika, maumivu ya tumbo na maumivu ya nyonga Maumivu wakati wa haja ndogo na kupata haja ndogo mara nyingi Kutoa uchafu kwenye mkundu, kuwashwa, maumivu au kutoa damu wakati wa haja kubwa Kukauka koo, kuwashwa, kumeza kwa shida au uvimbe kooni Maumivu kwenye macho, kutopenda mwanga mkali na/au kutoa uchafu kwenye macho unaofanana na usaha Kuvimba na joto kwenye maungio ya mifupa

Madhara Ya Kisonono

Kisonono ambayo haikutibiwa inaweza kuleta madhara makubwa na ya kudumu kwa jinsia zote.
Kwa wanawake, kisonono ambayo haikutibiwa inaweza kusababisha – pelvic inflammatory disease (PID) – ambayo inaweza kuharibu mirija ya uzazi na mara nyingine kusababisha ugumba. Kisonono ambayo haikutibiwa inaweza pia kusababisha mimba kutungwa nje ya nyumba ya uzazi (ectopic pregnancy), hali ambayo inaweza kumhatarishia mwanamke maisha yake.

Kisonono kinaweza kumsababishia mwanamke kuzaa njiti (mtoto kuzaliwa kabla ya siku) au mimba kuharibika.
Mwanamke mwenye kisonono anaweza kumwambukiza kichanga wakati wa uzazi na kukisababishia kichanga upofu wa kudumu,
maambukizi kwenye maungio ya mifupa au maambukizi kwenye damu.

Mwanamme ambaye ana kisonono isiyotibiwa anaweza kupata maumivu makali kwenye mapumbu kutokana na ugonjwa uitwao
epididymo- orchitis na kumsababishia ugumba.
Kisonono ambayo haikupewa tiba ya kutosha inaweza kumletea madhara kwenye tezi dume (prostate) na anaweza kupata makovu ndani ya mrija wa kutolea mkojo nje (urethra) na kufanya mkojo utoke kwa shida.
Kisonono huweza kusambaa hadi kwenye mifupa na damu hali ambayo ni hatari kwa maisha.

Tiba Ya Kisonono

Endapo vipimo vimeonyesha kuwa una kisonono, wewe na mwenzi wako wote mnatakiwa kutibiwa kwa kutumia antibiotics na kuacha kujihusisha na masula ya mapenzi hadi hapo tiba itakapokwisha. Baada ya kumaiza tiba, inashauriwa kujipa mapumziko ya angalau miezi 3 kuhakikisha kuwa maabukizi yote yamekwisha.

Ndugu msomaji, jisikie huru kuuliza maswali au kutoa maoni uliyo nayo kuhusu mada yetu ya leo, tutafurahi kuona tumekujibu vizuri.
By
Pharmacist Baraka J Makali

UGONJWA WA PUMU (ASTHMA)Utangulizi      Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye...
09/06/2018

UGONJWA WA PUMU (ASTHMA)

Utangulizi
Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu ya binadamu zinazojulikana kitaalamu k**a
bronch
Mtu mwenye pumu huwa na mcharuko mwili sugu (chronic Inflammation) kwenye mirija yake ya
kupitishia hewa (bronchioles tubes) hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija hii, kujaa kwa ute mzito (mucus) na kupungua kwa njia ya kupitishia hewa, hali ambayo humfanya muathirika kushindwa kuvuta na kutoa hewa
nje na hivyo kupumua kwa shida sana. Hali hii inaweza kudumu kwa muda mfupi au mrefu kiasi cha kuhitaji tiba ili kumuwezesha mgonjwa kupata nafuu. Kutokana na kuwepo kwa msuguano na uzuiaji wa kupitisha hewa wakati wa kupumua hwa nje, pumu hujulikana pia k**a obstructive lung disease .
Mtu aliye na pumu, huwa nayo kipindi chote cha maisha yake.

Makundi ya Pumu
Pumu inaweza kugawanywa katika makundi mawili;

Pumu ya ghafla (Acute asthma) :
Wagonjwa wanaopatwa na kundi hili la pumu huwa na hali ya kawaida katika njia zao za hewa isiyobadilika kati ya shambulizi moja na jingine.

Pumu sugu (Chronic Asthma) :
Kundi hili la pumu huwa na tabia ya kuwa na njia nyembamba za kupitisha hewa na kadiri jinsi mgonjwa anavyoendelea kupata matukio zaidi ya pumu, njia za hewa huzidi kuwa nyembamba zaidi.

Aina za ugonjwa wa pumu
Bila kujalisha mgonjwa anaingia katika kundi gani, ugonjwa wa pumu in awe a kugawanywa katika aina kuu nne,
ambazo ni
1.Pumu inayobadilika (brittle asthma) : Kulingana na tabia ya kujirudia rudia kwa matukio ta ugonjwa huu na madhara yake kwa mgonjwa, aina hii ya pumu inaweza kugawanywa zaidi katika aina nyingine mbili, ambazo ni:-

Aina ya kwanza ya pumu inayobadilika (type 1 brittle asthma) ni pumu yenye tabia ya kuwa na matukio na mashambulizi ya kubadilika kila mara japokuwa mgonjwa anaweza kuwa anapata matibabu kadhaa.

Aina ya pili ya pumu inayobadilika (type 2 brittle asthma) ni pumu ambayo mgonjwa anatokea kupata shambulizi la ghafla
(asthmatic attack) wakati hapo awali ugonjwa wake uliweza kuthibitiwa kwa matibabu.

2 ni utawalaPumu hatari isiyobadilika
(status asthmaticus) : Hii ni aina ya pumu iliyo hatari zaidi kwa mgonjwa. Pamoja na
matumizi ya dawa kadhaa,zikiwemo vitanua njia za hewa (bronchodilators) na vipoza mcharuko mwili (steroids) , mgonjwa wa aina hii ya pumu anaweza asipate nafuu ya haraka, na anaweza kupoteza maisha.

3 ni Pumu inayosababishwa na mazoezi
(Exercise Induced Asthma) :
Hali hii husababishwa na ufanyaji wa kupitiliza wa mazoezi ya viungo. Kwa kawaida wakati wa kufanya mazoezi mtu hupumua kwa kutumia pua na kupitia mdomoni. Hata hivyo wakati
mwingine hutokea hewa aivutayo huingia ndani ikiwa haijapozwa vya kutosha puani na hivyo kusababisha ongezeko la mtiririko wa damu katika mishipa inayosambaza damu katika mirija ya kupitisha hewa. Hali hii husababisha kuvimba
kwa kuta za mirija hiyo na muhusika kupata shambulizi la pumu. Aina hii ya pumu yaweza kudhibitiwa na dawa. Inashauriwa sana kwa watu wenye matatizo k**a haya kupasha moto misuli kwa mazoezi mepesi (warming up) kabla
ya kuanza mazoezi mazito na ya muda mrefu.

4 ni Pumu inayosababishwa na aina ya kazi afanyayo muhusika
(Occupational Induced Asthma) :
Wakati fulani, mazingira ya kazi yanaweza kusababisha kutokea kwa pumu hata kwa baadhi ya wafanyakazi wasio na tatizo hili. Mara nyingi aina hii huweza kuwatokea watu wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza matairi, vigae, rangi, kemikali mbalimbali, mbolea, chuma, unga na mbao.

Pumu husababishwa na nini?

Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha kutokea kwa pumu au yanayohusishwa na shambulizi lake. Mambo hayo ni pamoja na

1. Matatizo ya kinasaba: Matatizo ya kinasaba yamehusishwa na kutokea kwa karibu asilimia 90 ya ugonjwa wa pumu hususani kipindi cha utoto.

2. Uvutaji wa sigara au tumbaku kipindi cha ujauzito pia unahusishwa na kusababisha pumu KwaZulu mtoto atakayezaliwa.

3. Maendeleo ya kiuchumi: Ugonjwa wa pumu umeonekana sana kwenye nchi zilizoendeleea kiuchumi ikilinganishwa na nchi zenye maendeleo na hali duni ya kiuchumi.

4. Magonjwa ya mapafu k**a bronchitis

5. Vyanzo vya mzio
(allergens) k**a vile vumbi, vinyesi vya wanyama na baadhi ya vyakula.

6. Uchafuzi wa mazingira k**a moshi na baadhi ya harufu kali.

7. Baadhi ya kemikali kwenye maeneo ya kazi hasa kwenye viwanda k**a vya rangi, chuma, sementi na vigae.

8. Baadhi ya wagonjwa wanaotumia dawa za kushusha shinikizo la damu zilizo katika jamii ya beta-blockers k**a vile
propanolol wapo katika hatari ya kupata shambulio la ugonjwa wa pumu.

9. Magonjwa kwenye mfumo wa kupumua yasabishwayo na baadhi ya virusi na bakteria k**a vile rhinovirus, Chlamydia pneumonia au Bordetella pertusis .

10. Matumizi ya mapema sana ya baadhi ya dawa hasa antibiotiki kwa watoto yanaweza kubadilisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na hivyo kumfanya mtoto kuwa katika hatari ya kupata pumu.

11. Ongezeko la msongo wa mawazo huweza kusababisha pumu na matatizo katika mfumo wa upumuaj

12. Upasuaji wakati wa kujifungua (caesarian section): Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa kujifungua kwa njia ya upasuaji huongeza uwezekano wa kupata pumu kwa vile njia hiyo yaweza kuathiri mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya maradhi.

13.Vihatarishi vya ugonjwa wa pumu
Uwezekano wa kupata ugonjwa wa pumu huongezeka iwapo mtu

1. Atakuwa na magonjwa ya mzio k**a vile magonjwa ya ngozi (eczema) au homa isababishwayo na aina fulani ya vumbi (hay fever)
2. Atavuta chavu (pollen) kutoka kwenye maua au miti
3. Atajihusisha na uvutaji sigara
4. Ana historia ya ugonjwa wa pumu au mzio kwenye familia
5. Utumiaji wa dawa aina ya
aspirin
6. Ana msongo wa mawazo
7. Ana uambukizi wa magonjwa ya virusi k**a rhinovirus
8. Mazoezi
9. Anaishi sehemu zenye baridi
10. Ana matatizo katika njia yake ya chakula
(Gastroesophageal reflux disease au GERD)

Dalili za ugonjwa wa pumu

Dalili za ugonjwa wa pumu ni pamoja na
1. Kuishiwa na pumzi na kupumua kwa shida
(shortness of breath)
2. Kutoa sauti k**a mtu anayepiga miluzi wakati wa kupumua (wheezing)
3. Kukohoa sana (chronic cough) hasa nyakati za usiku au asubuhi. Aidha kikohozi huambatana na kutoa makohozi mazito, yasiyo na rangi au yenye rangi ya njano.
4. Kubana kwa kifua.
5. Kwa mtu aliyepata shambulizi kubwa la pumu (severe asthmatic attack) anaweza kushindwa kuzungumza na pia kuwa na hali k**a ya kuchanganyikiwa.
6.
Vipimo na Uchunguzi [​IMG]
Pamoja na daktari kutaka kufahamu historia ya mgonjwa, anaweza pia kuamua kufanya vipimo vifuatavyo ambavyo vitamsaidia kufahamu chanzo na madhara ya ugonjwa wa pumu kwa muathirika.
1. Kipimo cha damu (complete blood count) msisitizo ukiwa kwenye wingi wa seli za damu aina ya eosinophils ambazo uhusika na kuwepo kwa shambulio la mzio.
2. Kipimo cha kuchunguza uwezo wa mgonjwa kutoa hewa nje mara baada ya kuivuta (spirometery) . Aina hii ya uchunguzi hufanyika kabla ya mgonjwa kupewa dawa kwa kutumia nebulizer.
3. Kipimo cha kuchunguza kiwango cha hewa ya oksijeni kilichopo kwenye damu ya mgonjwa
(oximetry) .
4. Kipimo cha kuchunguza uwezo wa mgonjwa kupumua hewa nje wakati wa shambulizi la pumu
(Peak flow meter).
5. X-ray ya kifua kwa ajili ya kutofautisha pumu na magonjwa mengine yenye dalili za kufanana k**a vile ugonjwa wa moyo
(congestive heart failure), magonjwa sugu ya kuziba kwa njia za hewa (COPD k**a vile chronic bronchitis na emphysema) na magonjwa mengine ya kuzaliwa k**a vile cystic fibrosis .
6. Kipimo cha mzio cha ngozi (skin allergy test) kwa ajili ya kutambua aina ya mzio inayomsababishia mgonjwa shambulizi la pumu.

Matibabu ya Pumu

Kwa ujumla matibabu ya pumu hujumuisha kuepuka visababishi vya ugonjwa huu na matumizi ya madawa kwa walio na hali mbaya. Aidha, kwa wanaopata ugonjwa huu kwa sababu ya msongo wa mawazo hupewa ushauri nasaha kwa ajili ya
kusaidia kutatua matatizo yanayowakabili. Vilevile inashauriwa kwa wenye tatizo hili, kuwa na dawa karibu muda wote kwa ajili ya matumizi pindi shambulizi litakapotokea. Pia inashauriwa sana kuepuka mazingira na hali za baridi ambazo
huweza kuchochea kutokea kwa shambulio la ugonjwa huu.

Matibabu ya kutumia dawa hujumuisha matumizi ya dawa za kusaidia kupunguza na kuondoa makohozi (expectorants) , dawa zinazosaidia kutanua mirija ya hewa (bronchodilators) , dawa za kuondoa mcharuko mwili k**a vile cortisone ya drip (hasa wakati wa dharura) au nebulizer, na dawa za kuzuia
mzio (antihistamine drugs) .

Hata hivyo, kuna matibabu ya ziada kulingana na hali ya mgonjwa pamoja na kundi na aina ya pumu inayomuathiri mgonjwa.
Kwa wagonjwa wenye pumu ya ghafla na wenye hali mbaya
(acute asthma) matibabu hujumuisha matumizi ya dawa za kutanua mirija ya hewa
(bronchodilators) pamoja na kuongezewa hewa ya
oksijeni, dawa za kutuliza mcharuko mwili (steroids) pamoja na dawa za kutuliza kukak**aa kwa misuli ya mwili
(intravenous muscle relaxants) . Aidha kwa vile mara nyingi shambulizi hili laweza kuwa la hatari sana, mgonjwa hulazwa
hospitali na huongezewa hewa ya oksijeni, na kwa wagonjwa wasioweza kupumua kabisa, husaidiwa kufanya hivyo kwa kutumia mashine maalum iitwayo (mechanical ventilator).

Kwa wagonjwa wenye pumu sugu, jambo la muhimu ni
kuepuka visababishi vya pumu na kuendelea na matumizi ya dawa zinazosaidia katika kutanua mirija ya hewa. Kwa wagonjwa wanaopata mashambulzi ya mara kwa mara wanaweza kushauriwa na daktari kutumia dawa kadhaa zikiwemo zile zinazopunguza mcharuko mwili (mast cell inhibitors, inhaled steroids au oral steroids) , pamoja na dawa za
kutuliza kukak**aa kwa misuli ya mwili (muscle relaxants).

Aidha ni vema pia kutibiwa na kuthibiti kutokea kwa magonjwa yote yahusuyo mfumo wa hewa. Matumizi ya chanjo ya magonjwa k**a influenza na
pneumococcal pneumonia nayo husaidia sana katika uthibiti wa kutokea kwa pumu.

Ni vema pia kuepuka matumizi ya dawa za jamii ya beta-blockers kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu na ambao pia wana.
Imeandaliwa na
By
Pharmacist Baraka Makali.

Muonekano wako unaongeza iman kubwa kwa mteja wako ... Ila nimesahau koti ....
07/06/2018

Muonekano wako unaongeza iman kubwa kwa mteja wako ...
Ila nimesahau koti ....

What is Hemorrhoid or Piles?The re**al and a**l blood vessels mostly veins are dilated and swollen because of prolonged ...
04/03/2018

What is Hemorrhoid or Piles?
The re**al and a**l blood vessels mostly veins are dilated and swollen because of prolonged straining while passing stool and bowel movement.

Increase pressure within vein is also observed during pregnancy.
Swollen painful vein of re**um and a**s is known as hemorrhoids or piles. Swollen veins may form internal or external hemorrhoid.

Is Hemorrhoid or Piles a Serious Disease?
No, hemorrhoid is a benign disease of veins of re**um and a**s. Hemorrhoid is also known as piles.
Hemorrhoids or Piles is inflammatory disease of a**l and re**al veins. Hemorrhoid causes severe bleeding during defecation.
Straining while passing solid stool causes tear in hemorrhoid veins resulting in bleeding. The hemorrhoid disease is very painful condition.

What is Internal Hemorrhoid?
Internal hemorrhoid is not seen during examination. The enlarged veins are felt during examinations.
The enlarged dilated veins lie within re**al and a**l passage along the mucosal wall.

Internal hemorrhoids are described in 4 grades
What are the 4 Grades of Internal Hemorrhoids?
Grade 1- The dilated veins are within the wall of the a**s and re**um.

Grade 2- Veins prolapses during bowel movement and retracts at rest.

Grade 3- Blood vessels prolapse during bowel function, straining and sneezing. The dilated and engorged blood vessels often prolapse through a**l sphincter. The prolapse veins do not retract to normal position.

Grade 4- The pr*****ed veins cannot be reduced manually and remains pr*****ed out of a**l sphincter.

What is External Hemorrhoid?
The a**l veins when hypertrophied, swollen and enlarged in size then protrudes out of a**l ca**l. The swollen veins are felt and seen during examination. The disease is recognized as external non-inflamed or inflamed hemorrhoids. Dilated vein outside a**s is known as external hemorrhoids. External hemorrhoids often are thrombosed and extremely painful.

What Causes Pain?
Solid stool when passes through narrow a**l sphincter causes laceration of the vein. The lacerated vein is exposed to atmosphere and eventually gets infected. The infected veins show signs of inflammation. Inflammation causes severe pain at rest and during bowel movement.

What Causes Bleeding?
The dilated vein occupies the a**l opening. Solid stool when passes through the a**l opening causes laceration and tear of the a**l and re**al veins. The tear causes bleeding.

What is a Thrombosed Hemorrhoid?
External hemorrhoids are dilated and enlarged veins. The blood flow in veins are obstructed and stagnated because of strangulation created by a**l sphincter. The venous drainage is compromised and results in slow blood flow. The obstruction of blood flow results in clotting of the blood within the veins. When hemorrhoid gets infected the thrombus inside the vein also gets infected. The infected thrombus causes severe pain.

Describe the Causes of Hemorrhoids or Piles?
Following Are the Causes-
Straining during bowel movements
Continuous and prolonged cough seen in upper respiratory tract disease
Obesity
Pregnancy
Constipation results in straining during bowel movements.
Narcotic medication causes constipation.
Ascites results in difficulties in defecations and results in straining.
What Are The Other Symptoms And Signs Of External Hemorrhoids?
External Hemorrhoids Symptoms and Signs Are As Follows-
Discomfort at rest
Moderate to severe pain during bowel movements
Itching
Bleeding during bowel movements.
Lump is felt around a**s.
What Are The Other Symptoms And Signs Of Internal Hemorrhoids?
Internal Hemorrhoids Lie inside the Re**um. Symptoms are as follows-
Moderate to severe pain during bowel movements
Bleeding during defecation
Lump is not felt around a**l opening,
Re**al dilated veins are felt during re**al palpation (re**al examination with fingers).
Severe straining during bowel movement can cause protrusion of engorged and swollen veins through a**l sphincter.
When Should I See The Doctor For Hemorrhoids or Piles?
You should see a doctor when you experience above symptoms. You could see primary care physician or specialist. Specialists who are experienced in treating hemorrhoid are General Surgeon or Proctologist Surgeon.
How Can One Avoid Getting Hemorrhoids or Piles?

You should know risk factors to avoid formation of Hemorrhoids or Piles.
Hemorrhoids or Piles Risk Factors Are As Follows-
Obesity
Constipation
Pregnancy
A**l Manipulation and Stretching
Low Fiber Diet
Narcotic Medications Causes Constipation

What Is The Treatment For Hemorrhoid or Piles?
Hemorrhoids or Piles treatment options are conservative, medication or surgery.
Conservative Treatment for Hemorrhoids or Piles Are As Follows-
High fiber diet
Rest
Clean the skin around the a**s with clean water and soap once or twice a day. Wipe the skin clean following bowel function.
Drink lots of water.

What Are The Medications Used To Treat Hemorrhoids or Piles?

Constipation- Laxative
Pain- NSAIDs
Topical Agents and Suppositories - Ingredients are as follows
Petroleum Jelly
Zinc Oxide
Lidocaine
Epinephrine

Steroid Ointment- Should be used for itching and pain for 7 to 10 days only.
What Are The Surgical Procedures To Treat Hemorrhoids or Piles?

Surgery For Hemorrhoids or Piles Include:
Rubber Band Ligation - Most of the protruded veins are isolated and ligated with rubber band.
Sclerotherapy- Phenol is a sclerosing agent. Phenol is injected in vein to cause inflammation and collapse of the vein.
Cauterization- Infrared cauterization of enlarged strangulated vein results in shrinkage of hemorrhoids.
Excision- Veins are isolated and surgically excised. Open end of the veins are sutures and ligated.
Ligation of Artery- Artery supplying the re**al and a**l venous plexus is dissected and ligated. The result is lack of blood flow into hemorrhoid veins that results in collapse of the vein.
Radiofrequency Hemorrhoidectomy- The renal vein plication and radiofrequency ablation of hemorrhoid veins is effective treatment and prevents need for hospitalization.

What Are The Complications Of Hemorrhoids or Piles?
Bleeding
Anemia
Infection
Embolism

How to Prevent Hemorrhoids or Piles?
Following Are the Guidelines to Prevent Formation of Hemorrhoids or Piles-

Avoid constipation and diarrhea
Eat fiber diet
Drink lots of water daily
Take laxative with narcotics
Daily exercise

Address

Sumbawanga

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Baraka Makali posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Baraka Makali:

Shortcuts

Share